Mjema azindua ujenzi soko jipya Kisutu...soma habari kamili na matukio360...#share
Na Abraham Ntambara, Dar es Salaam
MKUU wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amezindua ujenzi wa
soko jipya la kisasa la Kisutu, jijini Dar es Salaam ambao unatarajia
kukamilika ndani ya kipindi cha miezi 18.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema (kushoto) na viongozi wa soko la Kisutu jijini Dar es Salaam, wakiwa wameshika ramani ya soko la kisasa linalotarajiwa kujengwa.
Akizungumza leo na wafanyabiashara wa Kisutu wakati wa uzinduzi
huo, Mjema amesema soko hilo litagharimu sh.bilioni 16 ambapo kwa sasa tayari
serikali imekwishawapatia sh.bilioni mbili kwa ajili ya kuanza kwa ujenzi huo
wa jengo la ghorofa nne.
“Taratibu zimekwishakamilika na tumeshampata mkandarasi, hivyo tutahakikisha
mkandarasi anajenga kwa ubora viwango na kwa muda tuliokubaliana au ikibidi
chini ya muda huo,” amesema Mjema.
Mjema amesema wakati wa ujenzi wafanyabiashara wa katika soko
hilo wataondolewa na kupelekwa maeneo mengine yaliyotengwa kupisha shughuli
hiyo ambapo amewahakikishia kuwa pindi utakapokamilika watapewa kipaumbele
katika kufanyabiashara.
Amesema Soko hilo likishakamilika litakuwa miongoni mwa masoko
bora mkoani Dar es Salaam .
"Soko hili likikamilika
litakuwa miongoni mwa masoko bora na la mfano,” amesema .
Aidha, mkuu huyo amewataka
wafanyabiasha walikuwepo sokoni hapo ambao wanapisha ujenzi wa soko kutoa ushirikiano
katika ujenzi ikiwemo kuondoka katika eneo ilo na kwenda kwenye maeneo
waliopangiwa na Halmashauri.
“Tunawaomba wafanyabiasha ninyi 633 mtoe ushirikiano katika
ujenzi ,Muende kwenye maeneo mliotengewa kwa Muda kwani Halmashauri imetenga
milioni 138 za kwenda kukarabati soko la mda la pale kisuto ambao watakwenda
wafanyabiashara za mboga,” ameongeza.
Ameleza kuwa wafanyabiashara wa nyama ya kuku wametakiwa kwenda
kufanyia biashara Mkunguni huku
wafanyabiashara wa mboga mboga na matunda wao wakiendelea kufanyia Kisutu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ilala, Msongela Palela amesema
ujenzi wa soko hilo ni wa Gorofa nne.
Amesema kuwa litakapokamilika litakuwa maeneo ya kufanyia
biashara, kupaki magari, kutakuwa na maeneo maalum ya Benki.
Aliyesimama ni Mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Ilala Msongela Palela, akizungumza wakati wa uzinduzi wa soko jipya la kisasa la Kisutu jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema akizungumza na wafanyabiashara wa soko la Kisutu jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi huo.
Ni sehemu ya wafanyabiashara wa soko la Kisutu jijini Dar es Salaam waliohudhuria katika uzinduzi wa soko jipya la kisasa la Kisutu.
No comments:
Post a Comment