Sakata la Nondo lachukua sura mpya, Zitto aingilia kati.....soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MBUNGE wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe amesema atampeleka Abdul Nondo uhamiaji Aprili 20, 2018 kama mbunge wa jimbo analotoka.
Hatua hiyo inakuja kufuatia Nondo kutakiwa kufika katika ofisi za uhamiaji ili kuhojiwa uraia wake.

Zitto kupitia ukurasa wake wa Facebook ameandika "Nitampeleka Abdul Nondo Uhamiaji tarehe 20/4/ 2018 kwa mamlaka yangu kama Mbunge wa Kigoma Mjini ( Jimbo analotoka Abdul na wazazi wake na mababu zake ),".

"Wananchi wa Kigoma Mjini waliopo Dar watakaotaka kunisindikiza Mbunge wao kumpeleka Abdul huko sitawazuia. Anyways, Mwami lazima asindikizwe,"amesema na kuongeza.

"Siku hiyo Uhamiaji watatuambia kama Kigoma sio Tanzania ili tuwaombe wasio wa Kigoma warudi Tanzania maana haiwezekani waliowengi pasiwe kwao na wachache ndio iwe kwao,,".

===========
Habari ndugu zangu wana TSNP.
Kwa muda wa takribani wiki moja mpaka sasa mwenyekiti wa TSNP Abdul Nondo amekuwa akihitajika uhamiaji ili akahojiwe kuhusu taarifa za uraia wake pamoja na za ndugu zake.
Hakupata nafasi ya kwenda sababu hakuwa sawa kutokana na changamoto alizokumbana nazo.
Jana pia tulipata wito kutoka uhamiaji ili tuweze kumpeleka na akahojiwe.
Jambo hilo tumelitimiza leo tar 4.4.2018. Baada ya kutoka mahakama kuu kwenye kesi yake ambayo imeahirishwa mpaka tar 11.4.2018.
Mnamo sa sita mchana tuliweza kumfikisha Abdul Nondo makao makuu ya ofisi za uhamiaji mkoa (makao makuu ya wizara ya mambo ya ndani)
Tulipata kuhoji alichoitiwa na anachotakiwa kujaza katika fomu aliyopatiwa.
Jibu tuliambiwa wanataka kupata taarifa zake binafsi, za wazazi wake, babu na bibi zake pande zote mbili (upande wa baba na upande wa mama) 
pamoja na za ndugu zake,kwani Afisa uhamiaji mkoa alitamka kuwa sheria inawaruhusu kumuhoji mtu yeyote wanaotilia mashaka uraia wake .nakuwa wanamashaka na uraia wa Abdul Nondo,hivyo awathibitishie kuwa yeye ni Raia wa Tanzania.
Amejaza taarifa zile anazozifaham tu.

Baada ya hapo afisa uhamiaji aliyekabidhiwa jukum la kumhoji Abdul Nondo alisema kwamba tar 20.4.2018 Abdul Nondo anapaswa kupeleka cheti chake cha kuzaliwa, cheti cha kuzaliwa cha baba yake, mama yake, cha bibi na babu mzaa baba na mzaa mama.
Asanteni.
©️ Paul Kisabo
Mwanasheria TSNP, Mkurugenzi wa Idara ya Sheria TSNP.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search