UVCCM Ilala wamtaka Waitara kujipanga sawa sawa 2020...soma habari kamili na matukio360...#share
Na Abraham Ntambara,
Dar es Salaam
UMOJA wa Vijana wa
Chama cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Ilala, umemtaka Mbunge wa Ukonga Mwita
Waitara kujipanga sawa sawa kwani haitakuwa rahisi kwake kurudi Bungeni 2020.
Katibu wa umoja huo Irene Mollel akizungumza na waandishi wa habari wakati wa semina jijini Dar es Salaam.
Kauli hiyo imetolewa
jana na Katibu wa umoja huo Irene Mollel akizungumza na waandishi wa habari
wakati wa semina kwa viongozi wao wa ngazi ya shina, kata na wilaya ya Ilala iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
“Kwa hiyo tunamwambia
ajipange sawa sawa vijana wa CCM wako imara, chama na jumuiya zake zote tatu
tuko imara, jumuiya hii kwa sasa tupo kikazi zaidi hatutaki mchezo,” amesema
Mollel.
“Jimbo la Ukonga tulilipoteza lipo upinzani, lakini
kwa sasa tunauhakika upepo uliotokea 2015 hautajirudia tena tutalichukua,”
amesisitiza.
AKizungumzia lengo la
semina hiyo, amesema lengo ni kuwaandaa viongozi wa wao ngazi ya mashina,
matawi na wilaya kujua majukumu yao ili kuhakikisha chama kinaendelea kushika
dola na hiyo ni kutokana na viongozi wengi walioingia katika jumuiya kuwa
wapya.
“Viongozi wengi
walioingia katika jumuiya baada ya uchaguzi ni wapya, kwa hiyo bila elimu hawawezi
kujua wajibu wao, hivyo tumeandaa semina hii kwa ajili ya kila mmoja kujua
wajibu wake ili kuhakikisha chama kinaendelea kushika dola,” amesema Mollel.
Amesema kuwa kama
wataendelea kutoa semina za jinsi hiyo CCM kitaendelea kushika dola kwa
asilimia 100.
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Ilala Hamad Pazzi akizungumza na waandishi wa habari wakati wa semina jijini Dar es Salaam.
Kwa upande wake Mwenyekiti
wa UVCCM wa wilaya hiyo Hamad Pazzi amesena metegemeo yao baada ya semina ni
kwamba viongozi wataweza kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa kanuni na katiba
ya CCM ili kusiwe na mwingiliano wakimamlaka katika ngazi mbalimbali.
Aidha aliwataka vijana wa
chama hicho kuwa wazalendo kwa kuhakikisha wanakuwa wa mfano katika kulinda amini
nchini.
Naye Mmoja wa watoa
semina Said King'emg'ena ambaye ni Katibu Msaidizi Mukuu wa Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu wa UVCCM kutoka makao makuu ya vijana, amesema huwa ni utalatibu wa CCM baada ya kufanya uchaguzi kuandaa semina
kwa ajili ya watendaji na viongozi kukijua chama chao, taratibu, misingi na
maadili ya chama chao.
Amesema kuwa kumekuwa
na changamoto ya kimaadili kwa baadhi ya viongozi wa chama ambapo hali hiyo
ilisababisha baadhi ya watu kuamini kuwa chama hicho kimekosa viongozi
waadilifu lakini kwa sasa chama
kimefanya kazi kubwa ya kurudisha nidhamu na maadili.
Matukio katika picha
No comments:
Post a Comment