VIDEO: Alichozungumza Mbowe baada ya kuachiwa kwa dhamana...tazama na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe amezungumza na waandishi wa habari kwa mara ya kwanza baada ya kuachiwa kwa dhamana yeye pamoja na viongozi wengine sita wa chama hicho na kusema kuwa walipokuwa magerezani wameshuhudia mengi na watayaweka wazi karibuni.

Mbowe amesema hayo alipokuwa nje ya Mahakama ya Hakimu mzaki Kisutu baada ya kukamilisha masharti dhamana ambapo kila mmoja alitakiwa kuwa na wadhamini wawili pamoja na kusaini bondi ya shilling Million 20.

"Leo mahakama imetupa ruksa ya dhamana na tunaanza dhamana yetu siku ya leo kwa mashtaka ambayo yananikabili mimi na wenzangu, tumekuwa gerezani Segerea kwa siku saba mimi na wenzangu na tunamshukuru Mungu tuko salama mimi na wenzangu na tumewaona Watanzania wengi zaidi ya elfu mbili ndani ya gereza la Segerea ambao wengi wao haki yao imecheleweshwa

"Kwa hiyo tunasema ni haki iliyominywa, tutazungumza mengi tuliyoyaona Segerea na baadaye tutatoa taarifa rasmi ya chama kuhusiana na kesi hii" alisema Mbowe

Msikilize hapo chini
 

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search