Sakata la Nondo kutekwa latua Bungeni...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Dodoma
MBUNGE wa CUF, Dk. Suleiman Ally Yussuf amehoji ni sababu zipi zilizofanya Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania
(TSNP), Abdul Nondo kuwekwa mahabusu ya Polisi kwa kipindi kirefu bila ya kufikishwa
Mahakamani kusomewa mashtka
Dk. Suleimani amehoji hayo leo katika Mkutano wa 11 wa kikao cha Bunge cha
kwanza kinachoendelea kufanyika katika mkoa wa Dodoma wakati alipokuwa anauliza
swali ya nyongeza kwenda kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba ambapo
alitaka kufahamu uhalali wa Jeshi la Polisi juu ya kuwashikilia watuhumiwa.
"Wako watu wengi wanaowekwa mahabusu ya Polisi kwa zaidi ya
siku 15 bila ya kupelekwa Mahakamani akiwemo mwanafunzi Abdul Nondo. Nataka
nijue ni sheria gani ambayo inatumika au inatumiwa na Jeshi la Polisi kuwaweka
watu mahabusu ya Polisi zaidi ya muda huo mrefu bila ya kupelekwa
Mahakamani", amehoji Dkt. Suleiman.
Aidha, katika kujibu hoja hiyo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mwigulu Nchemba amesema polisi ni chombo kilichoundwa kwa mujibu wa katiba na
sheria na linatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Katiba.
"Polisi wana mamlaka kisheria kutuhumu, kukamata, kuhoji na
kuweka watuhumia mahabusu kwa muda ulioruhusiwa kisheria endapo itabainika kuwa
kuna viashiria au taarifa ya kuhusika katika kutenda kosa la jinai.
"Kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za utendaji
zinazoongoza Jeshi la polisi inapobainika askari amembambika kesi kwa sababu
zozote zile huchukuliwa hatua mbalimbali za kinidhamu ikiwemeo
kufukuzwa",amesema Waziri Mwigulu.
Pamoja na hayo, Waziri Mwigulu ameendelea kwa kusema "kwa
kuwa jambo la kiusalama ni kipaumbele, kwa mtuhumiwa na rai wengine waliosalia,
Jeshi la Polisi hutumia wajibu wake waliopewa wa kulinda usalama wa raia kwa
kuweza kuhakikisha kwamba linatimiza majukumu yake na huku likiwaacha watu
wakiwa salama kabisa".
Kwa upande mwingine, Waziri Mwigulu hakuweza kujibu suala lolote
kuhusu Nondo kama jinsi lilivyo hojiwa na Mbunge Sulleiman juu ya uhalali wa
Jeshi la Polisi kumuweka kijana huyo zaidi ya siku 15 mahabusu ya polisi.
No comments:
Post a Comment