Wagonjwa 19,371 watibiwa JKCI Januari hadi Machi...soma habari kamili na matukio360...#share
Na
Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
TAASISI ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kipindi cha miezi mitatu ya Januari hadi Machi
2018 imeona jumla ya wagonjwa 19,371 wenye matatizo mbalimbali ya moyo kati ya
hao wagonjwa wa nje ni 18,481 na waliolazwa ni 890.
Kwa mujibu
wa taarifa iliyotolewa leo na kitengo cha uhusiano JKCI, wagonjwa 105
walifanyiwa upasuaji wa moyo wa kufungua kifua kati ya hao watu wazima 53 na
watoto 52. Kati ya wagonjwa 105 waliofanyiwa upasuaji 66 walifanyiwa na
madaktari wetu bingwa wa magonjwa ya moyo watoto wakiwa ni 35 na watu wazima
31.
Upasuaji wa
moyo wa bila kufungua kifua (Catheterization) kwa kutumia mtambo wa Cathlab
ulifanyika kwa wagonjwa 231 kati ya hao watoto ni 20 na wakubwa 211. Kati ya
wagonjwa 231 waliotibiwa wagonjwa watu wazima 211 walifanyiwa upasuaji na
madaktari wetu wa ndani.
Kwa kipindi
cha miezi mitatu tumekuwa na jumla ya kambi za matibabu nane (8) ambapo
tulifanya matibabu kwa kushirikiana na washirika wetu kutoka nchi za Ujerumani,
Israel, Australia , Marekani, India na Falme za Kiarabu. Katika kambi hizo
jumla ya wagonjwa 39 walifanyiwa upasuaji wa kufungua kifua kati ya hao watoto
17 na watu wazima 22. Wagonjwa 72 walifanyiwa upasuaji wa bila kufungua kifua
kati ya hao watoto 20 na watu wazima 52.
Tumefanya
upasuaji wa kuunganisha mishipa ya damu (AVF- Arterio Venous Fistula) kwa ajili
ya kusafishia damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo (Hemodialysis) 36.
Changamoto
kubwa tunayokabiliana nayo ni wagonjwa wengi tunaowapokea mioyo yao kutokuwa
katika hali nzuri hivyo basi tunawaomba wananchi kujenga tabia ya kupima afya
zao mara kwa mara hii itawasaidia kujuwa kama wana matatizo ya moyo au la na
kama wanamatatizo wataweza kupata tiba kwa wakati.
Wazazi na
walezi tunawaomba wasisahau kupima afya za watoto wao pale watakapoona kuna
hali ya tofauti katika ukuaji wa mtoto kwani magonjwa mengi ya moyo yanaanzia
utotoni. Mtoto akianza kuuguwa magonjwa ya moyo wazazi wengi wanadhani ni
matatizo ya kifua baada ya kumfikisha Hospitali na kufanyiwa vipimo ndipo
inagundulika mtoto anasumbuliwa na magonjwa ya moyo. Kwa wamama wajawazito
wafanye uchunguzi (Fetal Echocardiography) wa kuangalia kama mtoto aliyeko
tumboni anamatatizo ya moyo.
Aidha kwa
upande wa gharama za matibabu Taasisi yetu imeyagawa katika makundi manne (4)
tuna wagonjwa wanaotibiwa kwa bima mbalimbali ambazo tumeingia makataba nazo.
Wagonjwa wanaolipia gharama zote wenyewe, wagonjwa wanaochangia kidogo huku
gharama zingine zikilipwa na Serikali. Kundi la mwisho ni wagonjwa ambao
hawalipii kabisa gharama za matibabu ikiwa watakidhi vigezo vyote vya
kutokulipa.
Huduma zetu
za matibabu ya moyo zinatolewa kwa watanzania wote wa Bara na Visiwani.
Ifahamike kwamba fedha za matibabu zinazolipwa na wagonjwa zinatumika kununua
vifaa tiba vya moyo kama mlango wa moyo (Valve), betri ya moyo (Pacemaker) na
vinginevyo.
Kutokana na
matibabu ya moyo kuwa ya gharama kubwa tunaendelea kuwasisitiza wananchi
wajiunge na mifuko ya bima za afya ambayo itawasaidia kulipa gharama za
matibabu pindi watakapohitaji kutibiwa. Pia itasaidia Hospitali yetu kuendelea
kujiendesha yenyewe kwa kushirikiana na Serikali na wadau wengine.
No comments:
Post a Comment