WAZIRI MKUU AKUTANA NA RAIS WA KAMPUNI YA STARTIMES ...SOMA HABARI KAMILI NA MATUKIO360...#SHARE
Na
Mwandishi Wetu, Dodoma
WAZIRI
Mkuu Kassim Majaliwa amekutana na Rais wa Makampuni ya StarTimes Group, Bw. Xin
Xing Pang na kufanya naye mazungumzo. Mazungumzo hayo ambayo yalilenga kuimarisha
Ushirikiano uliopo baina ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na Kampuni ya
Star Media (T) Ltd.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Makampuni ya StarTimes Group, Bw. Xin Xing Pang walipofanya mazungumzo mjini Dodoma.
Katika
mazungumzo hayo Mhe. Majaliwa alionyesha kufurahishwa kwake na Ushirikiano
uliopo baina ya StarTimes na TBC na kuelezea matarajio yake juu ya Ushirikiano
huo. “Nina matarajio makubwa sana na Ushirikiano huu kwa sababu kupitia
Ushirikiano huu TBC itaimarika zaidi na kuwa na teknolojia bora zaidi”.
Rais
wa StarTimes, Bw. Pang alifika nchini kwa ajili ya kusainiana Mkataba wa
Makubaliano (MoU) na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC). Utiaji saini huo
ulishuhudiwa na Waziri mwenye dhamana ya Habari Mhe. Harrison Mwakyembe ambaye
naye pia aliongelea upande wa Wizara anayoisimamia, “Sasa kwa upande wetu kama
Wizara ni wajibu wetu kuhakikisha yote tuliyokubaliana yanatekelezwa”.





No comments:
Post a Comment