Gambo afiwa na mama yake...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu

MAMA mzazi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amefariki usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya The Madras Medical Mission – Chennai nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu.

Gambo kupitia mtao wake wa Instagram amethibitisha kifo hicho huku akieleza kuwa anahiaji maombi kwasababu huo ni mtihani mzito sana kwake.

"Kwa masikitiko na uchungu mkubwa napenda kutangaza kifo Cha Mama yangu Mzazi ( Mama aliyenilea kwa kuuza uji) kilichotokea usiku wa leo kwenye hospitali ya The Madras Medical Mission – Chennai nchini India! 

"Kama mtoto nilijitahidi kufanya kila lililowezekana ikiwa ni pamoja na kumpeleka Afrika Kusini kwa matibabu kabla ya India. Ni Imani yangu kuwa hata Mungu atakubali kuwa kama binadamu nilifanya kila lililowezekana Ila yeye kampenda zaidi! Niombeeni sana maana mtihani huu ni mzito sana kwangu sidhani kama nita uhimili!"

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search