IGP Sirro "feki' atiwa mbaroni...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Njombe
MTU mmoja aliyetambulika kwa jina la Maricha
Mniko(30) Mkurya dereva na mkazi wa Tandala Wilayani Makete anashikiliwa na
jeshi la polisi Mkoani Njombe kwa tuhuma za kujifanya ni Mkuu wa Jeshi la
Polisi nchini, IGP Simon Sirro ili kumsaidia ndugu yake kupata kazi katika
kampuni ya magari ya Japanisee.
Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Njombe, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Renata Mziga ambapo amesema kuwa tukio
hilo limetokea Mei 18 mwaka huu ambapo mtuhumiwa anadaiwa kumpigia simu Daniel
Junishi mmiliki wa kampuni ya magari ya Japanisee.
Kamanda Mziga amesema kuwa baada ya kumpigia
mtuhumiwa huyo inadaiwa alijitambulisha kuwa ni mkuu wa jeshi la polisi nchini
hivyo anatakiwa amwajili mdogo wake aliyeko mkoa wa Mara.
“Baada ya kumwambia huyu mmiliki wa magari ya
Japanisee alimuuliza kuwa namba yangu umeipata wapi akajibu nimepewa na Kamanda
wa Polisi Mkoa Njombe na akasema yupo Dodoma,”amesema Kamanda Mziga.
Aidha, Kamanda Mziga ametoa rai kwa wananchi
Mkoani humo kuwafichua watu wanaopiga simu kwa kutumia majina ya viongozi kwa
maslahi yao binafsi.
No comments:
Post a Comment