Magufuli atoa maagizo haya baada ya kupokea ripoti uhakiki mali za CCM...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) Dr. John Magufuli leo May 21, 2018 amepokea
ripoti ya tume aliyoiunda kuhakiki mali za chama hicho, iliyowasilishwa na
Mwenyekiti wa tume hiyo Dr. Bashiru Kakurwakatika ofisi
ndogo ya CCM Lumumba Dar es Salaam.
Kamati
hiyo imefanya kazi kwa miezi 5 ambapo imekusanya taarifa, imehakiki na
kuchambua taarifa na nyaraka zenye maelezo kuhusu idadi, aina na hali ya mali
zinazomilikiwa na kusimamiwa na chama, imeangalia vyanzo vya udhaifu wa mifumo
na taratibu za usimamizi wa mali.
Mwenyekiti
wa tume hiyo Dr. Kakurwa amesema uhakiki huo umefanyika kwa kutembelea maeneo
yenye mali za chama, kuwahoji watu mbalimbali wakiwemo viongozi waliohusishwa
na mali zilizokuwa zikihakikiwa, upitiaji wa nyaraka na kufuatilia uhalisia
katika ofisi za mamlaka husika, kufanya uchambuzi wa taarifa na kutoa
mapendekezo.
Ameongeza
kuwa uhakiki huo umefanyika katika mali za chama zilizo chini ya baraza kuu,
jumuiya za chama na kampuni za chama.
Katika
ripoti hiyo Dr. Kakurwa amesema tume imebaini uwepo wa upotevu mkubwa wa mali
za chama uliosababishwa na mikataba mibaya, ubadhilifu, wizi, usimamizi mbaya
wa mali, utapeli na ukosefu wa maadili katika uendeshaji wa miradi ya
chama.
Dr. Magufuli ameipongeza tume hiyo kwa
kazi kubwa iliyoifanya na amesema ripoti hiyo itawasilishwa katika vikao vya
Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM kwa ajili ya kufanyiwa uamuzi.
“Nilipokuwa nateua tume
hii nilikuwa najua ugumu wa kazi, nilikuwa najua kuwa mtapata shida kwenda
kuwahoji watu licha ya kwamba niliwapa uhuru wa kumhoji mtu yeyote na mmefanya
kazi nzuri sana, kilichobaki sasa ni kuifanyia kazi”amesema Rais Magufuli.
Rais Magufuli amewaagiza wajumbe wa
sekretarieti ya CCM waliohudhuria wakati wa uwasilishwaji wa ripoti hiyo kuanza
kufanyia kazi baadhi ya mambo yaliyo ndani ya uwezo wao na kwamba masuala
mengine yataamuliwa na vikao vikuu vya chama.
Kabla ya
kuondoka katika ofisi ndogo za CCM Lumumba, Dr. Magufuli amesalimiana
na wananchi waliokuwa nje ya ofisi hiyo na kuwahakikishia kuwa CCM imeamua
kuhakiki mali zake ili kukiwezesha chama hicho kulinda mali zake na kunufaika
na mali hizo.
Rais Magufuli amesisitiza kuwa CCM
imeamua kuchukua hatua hiyo ikiwa ni utekelezaji wa dhamira yake ya kupiga vita
rushwa na ufisadi na amewaeleza kuwa tume ya Dr. Kakurwa imefanya kazi nzuri.
“Huwezi ukaanza kupiga
vita rushwa na ufisadi ndani ya Serikali wakati chama kina rushwa na ufisadi,
chama nacho tunataka tukisafishe, mambo ya rushwa na ufisadi yaishe ili
Tanzania iende vizuri,” amesema.
“Ndio maana tumeunda tume
ya Dkt. Bashiru Ally, imefanya kazi nzuri sana, na ripoti hii tutaipeleka
Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ndani ya mwezi huu ili tuijadili na viongozi
watoe maelekezo” amesisitiza .
No comments:
Post a Comment