Kinana akabidhi ofisi...soma habari kamili na matukio360...#share

KATIBU Mkuu mstaafu wa CCM, Abdulrahman Kinana leo Alhamisi Mei 31, 2018 amemkabidhi ofisi mrithi wake, Dk Bashiru Ally katika ofisi ndogo za chama hicho tawala, Lumumba jijini Dar es Salaam.

Baada ya makabidhiano hayo, wawili hao waliingia katika kikao cha ndani na wafanyakazi wa chama hicho.

Dk Bashiru anakuwa Katibu Mkuu wa nane wa CCM baada ya kujiuzulu kwa Kinana aliyemuandikia barua mwenyekiti wa chama hicho, Rais John Magufuli aridhie ombi lake hilo.

Mei 29, 2018 Halmashauri Kuu, ambayo ni chombo cha pili kwa ukubwa cha CCM na ambayo ilikutana kwa siku mbili Ikulu jijini Dar es Salaam, ilimpitisha Dk Bashiru ambaye aliongoza kamati iliyohakiki mali za chama hicho kwa miezi mitano kuwa katibu mkuu mpya wa chama hicho.



About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search