Magufuli apewa daraja mto Kilombero...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Morogoro

RAIS John Magufuli amezindua daraja la mto Kilombero ambalo kwa sasa linaitwa daraja la Magufuli.

Akitangaza jina la daraja hilo leo Mei 5 wakati Rais akizindua, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema ametoa jina hilo kutokana na juhudi alizozifanya Rais Magufuli wakati akiwa waziri wa ujenzi.

"Mheshimiwa Rais kwa mamlaka niliyopewa natangaza rasmi daraja hili litaitwa Magufuli, hii ni kutokana na juhudi kubwa uliyoiweka katika kufanikisha ujenzi wa daraja hili," amesema.

Daraja hilo lenye urefu wa zaidi ya mita 300 linaunganisha wilaya za Ulanga, Malinyi na Kilombero.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search