Makamba: Nchi yetu inakabiliwa na changamoto kubwa ya uhifadhi wa mazingira...soma habari kamili na matukio360...#shsre

Na Abraham Ntambara,
Dar es Salaam
WAKATI tukielekea
katika maadhimisho ya siku ya mazingira duniani, Tanzania inakabiliwa na
changamoto kubwa katika uhifadhi wa mazingira ambapo asilimia 61 ya nchi
inakabiliwa na jangwa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) January Makamba akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam, juu ya maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani ambayo hufanyika Juni 5 kila mwaka.
Hayo yamebainishwa leo
jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na
Mazingira) January Makamba alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya
maadhimisho hayo ambayo huadhimishwa Juni 5 kila mwaka.
“Tukielekea kwenye
maadhimisho ya siku ya Manzingira Duniani, hali ya uhifadhi wa mazingira nchini
inachangamato kubwa, asilimia 61 ya nchi yetu inakabiliwa na jangwa,” amesema
Makmaba.
Amesema sababu ya hali
hiyo nikutokana na kilimo, ufugaji na uvuvu usioendelevu ambao umepelekea upotevu wa viumbe hai, kuaharibiwa kwa vyanzo
vya maji, kupunguwa kwa tija za shughuli za uzalishaji mali na uharibifu wa
mazingira.
Ameeleza kuwa hali hiyo
imepelekea hata kutokea kwa magonjwa amabyo ahayakuwepo ambapo alitoa mfano ni
kuwepo kwa ugonjwa wa malaria katika maeneo ya milimani tofauti na awali.
Akizungumzia maadhimisho
hayo, waziri Makamba amesema lengo ni
kuelimisha jamii, masuala mbalimbali yahusuyo mazingira, kuhamasisha jamii
kushiriki kikamilifu kwenye shughuli za maadhimisho hayo, kuhamasisha jamii
kuwa mstari wa mbele kuchukua hatua za kuhifadhi na kulinda mazingira ya maeneo
yao.
Makamba amesema lengo
la maadhimisho haya kitaifa kufanyika jijini Dar es Salaam ni kuwapa fursa
wananchi wa jiji hilo ya kuelemishwa na kuhamasishwa kupambana na changamoto za
uharibifu wa mazingira unaolikumba jiji hilo kama vile, mafuriko, uchafuzi wa
mazingira utokanao na plastiki, kubomoka kwa kuta za fukwe za bahari ya hindi
pamoja na utumiaji wa kiasi kikubwa cha nishati ya mkaa.
Amesema kutokana na
changamoto mbalimbali zinazokabili uhifadhi wa mazingira nchini, kuelekea siku ya
maadhimisho hayo kutatanguliwa na wiki ya mazingira itakayo zinduliwa na Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa Mei 31 hadi Juni 5, 2018 katika viwanja vya Mnazi Mmoja na
kutakuwepo na maonesho ya nishati mbadala ya mkaa na Teknolojia.
Ameongeza kuwa
wajasiriamali na wataalamu wa teknolojia ya nishati mbadala wa mkaa watatoa
mafunzo kwa jamii na kuwahamasisha kutumia nishati mbadala ya mkaa na
maadhimisho hayo yatafungwa na Rais John Magufuli siku ya kilele Juni 5, 2018.
No comments:
Post a Comment