Chadema yavua wawili uanachama...soma habari kamili na matukio360...#share

MWENYEKITI wa Baraza la Vijana la Chadema, Patrick Ole Sosopi, ametangaza kuwafuta uanachama wanachama wawili wa chama hicho.

Waliofutwa uanachana ni pamoja na aliyekua Naibu Katibu Mkuu Bara, Getrude Ndibalema na Mwenyekiti wa Bavicha mkoa wa Kilimanjaro, Dickson Kibona.

Akizungumza jana Mei 21, katika mkutano na waandishi wa habari jijini Arusha, Ole Sosopi alisema kwamba uamuzi huo umekuja baada ya kufuata taratibu zote za kuwahoji kupitia tume iliyoundwa.

Alisema viongozi hao wamehojiwa baada ya kuwepo tuhuma za usaliti ambalo ni kosa kubwa kwenye chama hicho.

Sosopi amesema Bavicha imeridhia kuwaondoa wanachama hao baada ya kujiridhisha kwa makosa waliyoyafanya.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search