Mrithi wa Kinana CCM huyo hapa...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
SIKU moja baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Tanzanzania John Magufuli kukubali ombi la aliyekuwa katibu mkuu wa chama hicho Abdulrahman Kinana ombi lake la kujiuzuru nafasi hiyo leo ametangazwa mrithi wake ambaye ni mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar es Salaam Dk. Bashiru Ally.
Itakumbukwa katibu huyo mpya alikuwa mwenyekiti wa tume maalumu iliyokuwa imeteuliwa na Rais Magufuli kwa ajili ya kukagua mali za CCM ambapo hivi karibuni walikamilisha kazi hiyo na kukabidhi ripoti kwa mwenyekiti wa chama hicho.
Kupitia taarifa iliyotolewa na Katibu wa itikadi na uenezi (CCM) Humphrey Polepole imesema kuwa Dk. Bashiru ameteuliwa kwenye kikao cha Halmshauri Kuu ya chama hicho ambacho leo ni siku ya pili kinaongozwa na Mwenyekiti ambaye ni Rais Dk. John Magufuli.
“Chama cha Mapinduzi kinapenda kuuhabarisha umma kuwa kupitia kikao chake ambacho kimekaa siku ya pili leo kimemteua Dk. Bashiru Ally kuwa katibu mkuu wa chama na ndugu Raymond Mangwala kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa chama cha Mapinduzi (UVCCM)”, imesema taarifa
Aidha Polepole amesema kuwa Rais amependezwa na kazi iliyofanywa na Tume iliyoongozwa na Dk. Bashiru ya uhakiki wa mali za Chama cha Mapinduzi.
No comments:
Post a Comment