Mwijage awekwa kikaangoni Bungeni...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

WAZIRI wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji, Mh. Charlses John Mwijage, amekosa uvumilivu wa kujibu swali la Mbunge wa Mpendae, Salim Hassan Turky (CCM),  kuhusu kwa nini sukari kwa upande wa Tanzania bara imekuwa ikiuzwa bei ghali tofauti na ilivyo Zanzibar.

Akiwa katika maandalizi ya kujibu swali hilo Mh. Mwijage amesema kwamba sababu ya sukari Tanzania bara kuuzwa ghali sana ni kutokana na gharama za uzalishaji bara kuwa juu sana kuliko Zanzibar jibu ambalo lilizua kelele nyingi za Wabunge.

"Mh. Spika nimejitahidi sana kuelezea suala hili lakini muda hautoshi....... Gharama za uzalishaji sukari bara zipo juu kuliko Zanzibar. Nimepewa muda naomba muache niwaeleze....Hili suala siyo rahisi kama mnavyofikiria.... Ndiyo siyo suala rahisi naomba niwaeleze," Mwijage akifafanua huku wabunge wakizidi kupiga kelele.

"I am very good in talking, I can talk....... Mh. Turky ulipopewa kibali na serikali kuingiza sukari ni kwa nini wewe hukuuza rahisi?"Ameongeza Mwijage.

Awali katika swali lake Mh. Turky alitaka kujua kwa nini viwanda vya Tanzania Bara vimekuwa vikishindwa kushusha bei za sukari ilhali Viwanda vya Zanzibar vinauza sukar sh 65000.

Akitolea mfano soko la dunia amesema kwamba "Sukari inauzwa dola 390  ukilipia kodi 25% na VAT 18% sukari inasimama kwa bei ya sh 65000. Watanzania wanalanguliwa kwa kuuziwa sukari 110000 kwa misingi gani"?

Pamoja na hayo Mbunge huyo amesema kwamba "Tulishaomba Cost of Production (Gharama za uzalishaji) hapa bungeni  tangu Naibu Waziri akiwa Malima na hatujaweza kuletewa mpaka leo" 

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search