StarTimes na SOS Children’s Villages zaunganisha nguvu kuwainua Vijana...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KAMPUNI ya matangazo
ya kidigitali ya StarTimes pamoja na SOS Children International zimesainiana mkataba
wa makubaliano jijini Nairobi. Mkataba huo utafanya Kampuni hiyo na vituo vya
SOS kushirikiana katika kusaidia familia na watoto wenye uhitaji, huku mkazo
zaidi ukiwa ni kuwawezesha vijana kutizimiza malengo ya Kimaendeleo ambayo kama
Umoja wa mataifa unavyohimiza.
Kupitia mkataba huo
StarTimes itakuwa ikisaidia program na miradi mbalimbali katika nchi zaidi ya
10 barani Afrika ili kukuza nafasi za kujifunza na kuongeza ujuzi zaidi kwa
vijana ambao wako katika programu za vijiji vya SOS.
Hii itajumuisha
mafunzo ya kiufundi na ujuzi pamoja na ushauri kwa vijana hawa huku wakipata
nafasi ya Matangazo ya Kidigitali katika vituo vyao. Hii itawanufaisha vijana
kuona fursa nyingi ambazo zinaambatana na matangazo ya kidigitali.
Akizzungumza katika
hafla ya kusainiana mkataba huo, Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Mahusiano Bw.
William Masy alisema kwamba Kampuni hiyo ilifikia uamuzi huu wakati wa Mkutano
mkuu wa YouthConnekt Afrika uliofanyika nchini Rwanda mwaka 2017. Vijiji vya
SOS vinatoa fursa kwa vijana kuingia moja kwa moja katika soko la ajira na
kujitengenezea kesho yenye tija.
“Kampuni ya
StarTimes imejipanga kuhakikisha inawawezesha vijana kushiriki moja kwa moja
katika shughuli za kimaendeleo kupitia programu mbalimbali za mafunzo na
malezi. Ndio maana ushirikiano huu ni zana kubwa katika kuelekea maendeleo
ambayo kila mmoja wetu anayataka, vijana hawa watakuwa na ujuzi wa kutosha
kukabiliana na changamoto ili kuendeleza jamii zao na vizazi vya baadaye,”
alisema Bw. Masy
Naye Naibu
Mkurugenzi Mtendaji wa SOS, Bi. Shubha Murthi alisema, “Ushirikiano kama huu
ndio hufanya kazi hii iwezekane.
Tunaweza kufikia malengo ya kusaidia vijana kutimiza ndoto zao kupitia
ushirikiano madhubuti wa Kampuni makini kama StarTimes. Matokeo ya kazi hii ni
bora na yenye tija”.
No comments:
Post a Comment