TFF yatangaza wachezaji 30 kuwania tuzo mchezaji bora...soma habari kamili na matukio360...#share

Na
Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
SHIRIKISHO
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)limetangaza majina ya wachezaji 30 katika
kuelekea mwisho wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) ambao
watawania Tuzo za Mchezaji Bora mwaka huu.
Akizungumza
leo jijini Dar es Salaam Msemaji wa TFF Clifford Ndimbo amesema utaratibu huo
hufanyika kila mwaka baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu ya Vodacom kwa
kushirikiana na Kampuni ya Simu ya Mkononi ya Vodacom.
Ndimbo
amefafanua wachezaji hao 30 watachujwa na kubaki 10 na baadae watabaki
wachezaji wa tatu wataoinga hatua ya fainali ili kumpata Mchezaji bora kwa
msimu huu.
Amewataja
wachezaji wanaowania tuzo hiyo ni Habibu Kyombo (Mbao),Khamis
Mcha,(RuvuShooting),Yahya Zayd(Azam),Razack Abalora(Azam), Bruce
Kangwa(Azam) Aggrey Morris(Azam),Himid Mao (Azam),Awesu Awesu(Mwadui) na Adam
Salamba(Lipuli).
Wengine ni
Mohammed Rashid(Prisons), Shafiq Batambuze(Singida),Mudathir Yahya (Singida),
Marcel Kaheza(Majimaji),Ditram Nchimbi(Njombe Mji) na Eliud Ambokile(Mbeya
City).
Pia Shaaban
Nditi(Mtibwa), Tafadzwa Kutinyu(Singida) Ibrahim Ajibu(Yanga), Gadiel
Michael(Yanga),Papy Tshishimbi(Yanga),Kelvin Yondani(Yanga),Obrey
Chirwa(Yanga),Aishi Manula(Simba), Emmanuel Okwi(Simba),John Bocco(Simba),
Jonas Mkude(Simba),
Erasto
Nyoni(Simba),Shiza Kichuya(Simba),Asante Kwasi(Simba),Hassan Dilunga(Mtibwa).
"Mchakato
wa kupata mchezaji bora unatarajia kufanyika Juni 23 mwaka huu katika Ukumbi wa
Mlimani City jijini Dar es Salaam. Ambapo msimu huu kutakuwa na washirika
wengine Azam Tv, Benki ya KCB na Premier Bet,"amefafanua
Pia amesema
licha ya tuzo ya Mchezaji Bora wa mwaka wa ligi, kutatolewa tuzo mbalimbali,
ambapo kwa mwaka huu tuzo moja imeondolewa na nyingine imeongezwa ikiwa ni
katika uboreshaji
"Tuzo
iliyoondolewa ni ya Mchezaji Bora wa Kigeni na imefanyika hivyo ili kuwapa
fursa wachezaji wote kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL badala ya
kuwatenganisha, vile vilee msimu huu imeongezwa Tuzo ya Mwamuzi Bora Msaidizi
ambayo haikuwepo msimu uliopita.Hiyo ni kutokana na kuthamini nafasi ya waamuzi
wasaidizi,"amesema Ndimbo
Kwa
mazingira hayo tuzo zitakazotolewa siku hiyo ambapo wadhamini wakuu ni Kampuni
ya simu za mkononi ya Vodacom ni Bingwa,Mshindi wa Pili,Mshindi wa Tatu,Mshindi
wa Nne, Mfungaji Bora,Timu yenye nidhamu,U20 Player (Tuzo ya Ismail
Khalfan),Mchezaji Bora Chipukizi, Mwamuzi Bora Msaidizi,Mwamuzi BoraKipa
Bora,Kocha Bora,Goli Bora VPL,Best Eleven,pamoja na Mchezaji wa heshima.
Ndimbo
amesema zawadi kwa kila kategori pamoja na majina ya wanaowania tuzo ukiacha
bingwa, mshindi wa pili, wa tatu, wa nne na mfungaji bora ambao hujulikana
kulingana na ligi inavyoendelea zitatangazwa siku za usoni.
"Kila
mwezi Kamati ya Tuzo, imekuwa ikitangaza jina la mchezaji aliyefanya vizuri kwa
mwezi husika kutokana na vigezo mbalimbali na pia ripoti kutoka kwa makocha
waliopo katika viwanja ambavyo ligi hiyo inachezwa.
"Wachezaji
ambao walishinda tuzo za mwezi ligi ya msimu huu ni nimshambuliaji wa
Simba, Emmanuel Okwi (Agosti), beki wa Singida United, Shafiq Batambuze
(Septemba) na mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa (Oktoba).
"Wengine
ni kiungo wa Singida United, Mudathir Yahya (Novemba), mshambuliaji wa Mbao FC
ya Mwanza, Habibu Kiyombo (Desemba), mshambuliaji wa Simba, John
Bocco(Januari), kiungo wa Yanga, Papy Tshishimbi (Februari), mshambuliaji
wa Lipuli, Adam Salamba (Machi) na mshambuliaji wa Majimaji, Marcel
Kaheza (Aprili),"amesema Ndimbo.
Ambapo
wachezaji hao kila mmoja amepewa zawadi ya tuzo, king'amuzi cha Azam na fedha
Sh.milioni moja kutoka kwa wadhamini Vodacom.
No comments:
Post a Comment