Chuo cha NIT chapandishwa hadhi ya chuo kikuu...soma habari kamili na matukio360...#share


Na Abraham Ntambara

SERIKALI imekipandisha hadhi Chuo  cha Usafirishaji nchini (NIT) kuwa chuo kikuu ambapo hivi karibuni kinatarajia kuanza  kutoa elimu ya shahada ya kwanza.


Pichani Kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Usafirishaji nchini (NIT),Profesa Zacharia Mganilwa,akikabidhiana makubaliano ya ushirikino baina ya Chuo hicho na Chuo cha Usafirishaji nchini Korea ,na Profesa Woo Jongwouk , ambaye alimwakilisha Profesa Lee Byungchan naye ni Rais wa Chuo kikuu cha Usafirishaji nchini Korea,makubaliano hayo yamefanyika leo Jijini Dar es Salaam.


Hayo yamebainishwa  leo Jijini Dar es Salaam na Mkuu wa chuo hicho, Profesa Zacharia Mganilwa, wakati wa halfa fupi ya kutiliana saini ya Ushirikiano baini ya Chuo cha NIT na Chuo cha Usafirishaji nchini Korea.

“Katika kuimarisha sekta ya usafirishaji nchini, serikali ilikipandisha hadhi chuo hiki ya kuwa chuo kikuu, na kitaanza kutoa elimu ngazi ya shahada,” amesema Profesa Mganilwa.

Akizungumzia kuhusu makubaliano walioingia baina ya vyuo hivyo, amesema makubaliano hayo ni kwa  ajili ya kutoa mafunzo kwa Walimu wa chuo cha NIT ili waweze kupata ujuzi wa jinsi ya kusimamia Usafiri wa Treni ambazo zinatumia Umeme.

Profesa Mganilwa ameongeza kwamba katika makubaliano hayo yatakisaidia chuo hicho  kutoa Walimu wenye shahada ya kwanza kwenda nchini Korea kusomea Shahada ya uzamili ya masuala ya usafirishaji wa Treni za kisasa.

"Katika makubaliano haya Walimu wenye Shahada ya kwanza watapata fursa ya kwenda nchini Korea kwenda kupata Ujuzi wa Masuala ya Usafirishaji wa Uendeshaji Treni za Umeme ili waje kutoa elimu kwa Vijana wetu hapa nchini"Amesema Profesa Mganilwa .

Profesa Mganilwa amesema Mafunzo hayo  kwa Walimu hao yanataisadia nchini kwa sasa ambapo inaingia katika usafiri wa Treni za kutumia mfumo wa  Umeme ambapo mradi wake unaanza kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro.
Amesema kwa sasa katika chuo hicho wana Walimu wachache wenye ujuzi wa kufundisha Wanafunzi katika uendeshaji wa Treni za Umeme.

"Hapa Chuoni tuna Walimu wachache wa hivyo kuongezeka kwa walimu hama kutasaidi kupanuka kwa ufundishaji  Wanafunzi hawa ambapo wataweza kusimamia hizi"Ameongeza kusema.

Hata Hivyo ,Profesa Mganilwa amesema makubalino hayo yanakuja ikiwa ni teyari Serikali imeshakipandisha Hadhi chuo hicho na kuwa cha Usafirishaji huku akiwaka wanafunzo wote wanaohitimu kidato cha nne na Cha Sita kuhakikisha wanajitokeza katika kusomea masomo ya usafirishaji wa njia ya Reli.

Kwa Upande wake, Profesa Woo Jongwouk , ambaye alimwakilisha Profesa Lee Byungchan naye ni Rais wa Chuo kikuu cha Usafirishaji nchini Korea,amesema wataendelea kushirikiana na Chuo cha NIT katika kutoa watalaamu mbali mbali katika usafirishaji.

"Tunafarijika na ushirikiano huu mzuri,na tunawahaidi tutaendelea kushirikiana na Chuo hichi katika kuzalisha wataalamu "Amesema Profesa Jongwouk.


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search