TIC yaandikisha miradi ya Dolla za Kimarekeni milioni 13 kwa miezi minne...soma habari kamili na matukio360...#share


Na Abraham Ntambara, Dar es Salaam

KITUO cha Uwekezaji nchini (TIC) kimesema kwa kipindi cha miezi minne kimeweza kuandikisha miradi mipya 109 ambayo inatarajiwa kuwekeza kiasi cha Dolla za Kimarekani zaidi ya milioni 13.
Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Geoffrey Mwambe akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho Geoffrey Mwambe alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya baadhi ya mafanikio ya TIC, amesema inatarajia kuajiri wafanyakazi wapya 18,172.

“Uwekezaji zaidi umefanyika katika sekta za ujenzi, uzalishaji viwanda,  usafirishaji, kilimo na miundombinu,” amesema Mwambe.

Mwambe amebainisha kuwa katika miradi hiyo 28 sawa na asilimia 34.86 inamilikiwa na wageni, miradi mitatu sawa na asilimia 2.75 ni ya ubia na miradi 68 sawa na 62.40 inamilikiwa na Watanzania.

Aidha amesema uchambuzi huo unaonesha kuwepo kwa mwamko mkubwa kwa wawekezaji wazawa katika sekta za viwanda, kilimo na miundombinu tofauti na ilivyozoeleka ambapo uwekezaji ulijikita katika sekta za utalii na usafirishaji wa mizigo.

Amewataka wakuu wa mikoa pamoja na wakuu wa wilaya na taasisi mbalimbali za kiserikali kukuza mazingira wezeshi ya uwekezaji ikiwemo kutenga maeneo ya kuwekeza.

Amesisitiza  wakuu hao wa mikoa , kufanya tasmini ya mara kwa mara ya kuhusiana na uwekezaji katika mikoa yao, ambapo amewataka kutowanyanyasa wawekezaji na kuboresha mazingira wezeshi kwa wafanyabiasha.

Amesema kuwa juhudi hizo zikfanyika kwa nguvu na msisitizo mkubwa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa sekta hiyo, kutawezesha kukuza uwekezaji nchini na kuibua fursa kubwa za ajira kwa vijana.

Ameeleza kwamba kama taasisi mbalimbali zitaweka jitihada kubwa katika kuwekeza kwenye sekta ya viwanda kutasaidia kupanua wigo wa walipa kodi, na hatimaye kuongeza uzalishaji na kufikia uchumi wa kati.

Amezitaka taasisi zote nchini pamoja na mamlaka zote husika kukuza ushirikiano na kituo hicho cha uwekezaji ili kuweza kujenga uelewa na kutoa miongozo kwa ajili ya kuweza kusimamia ujenzi wa viwanda nchini.

Mkurugenzi  huyo  amesema kuwa kituo chake kimeongeza ofisi nne mpya za kanda katika mikoa ya Dodoma, Dar es salaam, Mtwara na kigoma ambazo ni kanda ya kati, wakati kanda ya mashariki vituo vilivyoongezwa ni pamoja na pwani na Dar es salaam.

"Uboreshaji wa huduma katika kituo cha uwekezaji unasaidiwa zaidi na mfumo uitwao (one stop facilitation Center) ndani ya ofisi zetu ambapo mfumo huo hutoa huduma za usajili wa makampuni pamoja na kodi" amwsema Mwambe.

Hata hivyo kituo hicho kinashirikiana na Serikali katika kutoa ushauri na kuboresha mazingira ya uwekezaji ambapo kulingana na Takwimu za Benki ya Rand Merchant (RMB) zilizotolewa mwaka 2015, Tanzania ilishika nafasi ya Tisa kati ya nchi kumi zenye ushawishi wa kuvutia waweze kuwekeza.



About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search