Wadau waunga mkono baadhi vipegele kanuni za maudhui ya mitandao...soma habari kamili na matukio360..#share
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
BAADHI ya wadau wameunga mkono baadhi ya vipengele katika kanuni za maudhui ya mitandao vyenye kulinda maadili
na utu.
Mmoja wa wa wadau wa mitandao ya kijamii akizungumza kuhusu mitandao ya kijamii inavyoweza kukuza utawala bora.
Hayo yanakuja wakati huu
ambao kumekuwa na malalamiko juu ya kanuni hizo mpya za maudhui ya mitandao
ambazo zimetolewa hivi karibuni na serikali kwani zinadaiwa kuminya uhuru wa
kujieleza.
Baadhi ya vipengele vinavyoungwa mkono vinahusu kulinda haki za
mtoto, kuzuia matusi mtandaoni na hata kupunguza picha zisizofaa.
Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na wadau mbalimbali
wakati wakichangia mdahalo ulioandaliwa na Kituo cha Sheria na Haki za binadamu
(LHRC) uliokuwa na lengo la kujadili mchango wa mitandao ya kijamii katika
kukuza utawala bora.
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Jamii Forums, Maxence Melo, Mkurugenzi wa Utetezi na Maboresho Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Anna Henga (katikati) na Mwanasheria wa LHRC, William Kahale wakiwa katika mdahalo huo.

Washiriki wa mdahalo huo wakifuatilia kilichokuwa kikiendelea.

No comments:
Post a Comment