Viongozi wa dini wahimiza jamii kutunza mazingira... soma habari kamili na matukio360....#share

Na Mwandishi Wetu,  Dar es Salaam

VIONGOZI wa dini nchini wameihimiza jamii kujenga utamaduni wa kuyatunza na kuyahifadhi mazingira kwa ajili ya ustawi wa vizazi vilivyopo na vijavyo.
Pia wameiomba Serikali kusisitisha matumizi ya mifuko ya plastic ili kupunguza uharibifu wa mazingira unaosababishwa na mifuko hiyo.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam kwa wakati tofauti na viongozi wa madhehebu wa dini wakati wa Mjadala wa Kitaifa kuhusu imani ya Dini na katika kuhifadhi mazingira katika wiki ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira itakayofikia kilele Juni tano mwaka huu katika Viwanja vya Mnazi Mmoja.

Akizungumza katika mjadala Padri wa Kanisa Katoliki, Raymond Saba amesema jamii inatakiwa kuvitengea haki vizazi vilivyopo na vijavyo kwa kuyatunza na kuyahifadhi mazingira na kwenda kinyume kumkosea Mungu muumba wa mazingira.

“ Tuvitendee haki vizazi hapa duniani hata Mwenyezi Mungu katika maandiko yake anaitaka jamii kuyatunza na kuyahifadhi mazingira hivyo kuyaharibu ni kumkosea,” amesema.

Amebainisha kuwa viongozi wa dini wanatakiwa kutumia miundombinu ya dini kuihimiza jamii kwa kuipa ujumbe wa utunzaji na uhifadhi mazingira.

Kwa upande wake, Askofu wa Kanisa la Kiinjili na Kilutheri Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Alex Malasusa ameikumbushia Serikali kuhimiza wananchi kuacha matumizi ya mifuko hiyo  kwani inachangia uharibifu wa udongo.

Amesisitiza kuwa kanisa hilo linashiriki kampeni ya utunzaji mazingira kwa kupanda miti zaidi ya 3000 kwenye vijiji na wilaya iliyopandwa na vijana katika wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.

Naye Mjumbe wa Baraza la Ulamaa-Baraza la Waislamu Tanzania, Sheikh Othman Issa amesema kuna uharibifu mkubwa wa mazingira ambapo kiasi cha tani milioni nane za plastiki zinatupwa baharini hali inayohatarisha ustawi wa viumbe.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba amesema Serikali iatayafanyia kazi mapendekezo mbalimbali ya utunzaji wa mazingira yaliyaowasilishwa na viongozi.
Katika hatua nyingine, amesema Serikali iko tayari kufanya kazi na vyombo vya habari vinavyomilikiwa na taasisi za dini katika masuala ya utafiti wa mbinu za utunzaji mazingira.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search