BREAKING NEWS!! WIZI WA MAFUTA YA 'BOMBADIA' WANNE WAPANDISHWA KIZIMBANI

MAFUTA YA 'BOMBADIA  YABURUTA WANNE KIZIMBANI!! PATA HABARI HII NA NYENGINE KUPITIA WWW.TANZANIAMPYAMATUKIO.BLOGSPOT.COM

NA: Mwandishi Maalum; Matukio.

Watu wanne wakiwamo maofisa wawili wa jeshi la polisi wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shtaka la uhujumu uchumi kwa kuchota Lita 280.6 za mafuta ya ndege ya ATCL.

Wakili wa Serikali , Nassoro Katuga aliwataja washtakiwa hao kuwa ni Mlinzi wa kampuni ya ulinzi ya Moko, Iddy Juma Nyangas (42), Askari F. 8419 Koplo, Bahati  Msilimini (33), F. 9901 ,PC Benaus (34) na Fundi Ndege,  Ramadhan Mwishehe (52).

Akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa,  washtakiwa hao wanaiwa kutenda kosa hilo kati ya Machi Mosi na 17,2017.

Alidai kuwa kati ya Machi Mosi na 17, 2017 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Jk Nyerere walichota Lita 280.6 za mafuta ya ndege Jet AI ya ATCL

Katuga alidai kuwa walichota mafuta hayo kutoka kwenye ndege hiyo  ya ATCL 5H-MWF-DASH8Q300.

Washtakiwa hawakuruhusiwa kuongea chochote kwa sababu wanakabiliwa na shtaka la uhujumu uchumi ambalo makama hiyo haina uwezo wa kulisikiliza. Na kesi hiyo itatajwa tena April 1, 2017

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search