Wajue maafisa Korea Kaskazini wanaotajwa kutengeneza makobora tishio ..soma habari kamili na matukio360..#share
Na mashirika ya kimataifa
Kim Jong-sik na Ri
Pyong-chol ambao ni maafisa wa Korea Kaskazini wamewekewa vikwazo na Marekani
ikidai wamechangia kuundwa kwa makombora
hatari ya nchi hiyo.
Maafisa wa Korea Kaskazini waliowekewa vikwazo na Marekani, Kim Jong-sik na Ri Pyong-chol
Wizara ya fedha nchini
Marekani imesema wote walikuwa viongozi wakuu katika mpango wa makombora ya
masafa marefu ya Korea Kaskazini.
Ijumaa iliyopita Baraza la
ulinzi la Umoja wa Mataifa liliiwekea vikwazo vipya Korea Kaskazini kujibu majaribio yake ya makombora ya masafa
marefu.
Hata hivyo Korea Kaskazini
ilisema hatua hiyo ni kama vita.
Vikwazo hivyo vipya vya
Marekani vitazuia shughuli zozote za wanaume hao wawili zinazofanywa nchini
Marekani, na hata kutwaliwa kwa mali yao iliyo nchini Marekani.
Wanaume hao wawili
wanaonekana mara kwa mara wakiwa na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un
wakiwa maeneo ya kuyafanyia majaribio makombora.
Mwaka huu nchi hiyo imefanya
majaribio kadha ya makombora tofauti ambayo inasema kuwa yanaweza kufika nchini
Marekani. Tayari nchi hiyo imetangaza
kuwa na mitambo ya kuzuia makombora
No comments:
Post a Comment