ETI NINI ?... "NEY WA MITEGO KUTINGA IKULU..."


Katika hatua iliyotafsiriwa kuwa ni kuwatoa 'khofu' wasanii wa kazi mbali mbali za sanaa, kitendo  cha Rais Magufuli  amemualika Ney wa Mitego Ikulu, kufanya Mazungumzo.
Baadhi ya wadau walikuwa na haya ya kusoma:

Hii inaweza kuwa faida kwa mwanamuziki kwani ni moja ya CV adimu sana kutokea.
Leo nasikia Ney naye kaitwa na mkuu akale bata.

Sipati picha msanii kama Ney kuingia Ikulu, nadhani ndio first time km ni kweli.
Source hawa hapa chini.

=========

Msanii maarufu kwa jina la Ney Wa Mitego


Msanii wa muziki wa kizazi kipya Emmanuel Elibariki maarufu kama Nay wa Mitego ameitwa Ikulu jioni hii kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Rais John Magufuli.

Nay amepata mwaliko huo ikiwa ni sasa chache baada ya kuachiwa huru na Jeshi la Polisi lililokuwa likimshikilia tangu jana.

Katika mahojiano yake na kituo cha Televisheni cha Azam Two, Nay alikiri kupata mwaliko huo na kueleza kuwa ataitumia vyema nafasi hiyo kumuelezea Rais Magufuli hali halisi ya maisha ya Watanzania.

“Nimepokea mwaliko bado nafikiria nini cha kuongea naye endapo nitapata hiyo nafasi ya kuzungumza naye, nadhani itakuwa nafasi nzuri ya kumweleza vile ambavyo Watanzania sisi tunaishi mtaani,”alisema.

Nay alikamatwa na polisi jana mkoani Morogoro na kusafirishwa hadi Dar es Salaam kwa kile kilichodaiwa kutunga wimbo wenye maudhui yanayoikashifu Serikali.

Mapema leo mjini Dodoma, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe alisema Rais Magufuli ameagiza msanii huyo aachiwe huru na wimbo wake uendelee kuchezwa na kusambazwa.

Chanzo: Mwananchi

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search