NAPE NNAUYE: 'KUMBE WEWE SHUJAA'

KATIKA HALI ILIYOWEKA UTAIFA MBELE, WAZIRI WA ZAMANI WA WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO...  AMEKABIDHI OFISI KWA WAZIRI MPYA WA WIZARA HIYO KATIKA TUKIO LILILOVUTIA NA LILILOWEKA UTAIFA KWANZA.
TANZANIA MPYA MATUKIO IMEKUSANYA TUKIO HILI NA KULILETA KWA KWA MSAADA MKUBWA WA MTU WA NGUVU!!

Aliyekuwa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamadunu na michezo, Nape Nnauye leo amekabidhi ofisi kwa Waziri Mpya wa Wizara hiyo, Dk. Harrison Mwakyembe. Makabidhiano hayo yamefanyika katika ofisi za Wizara Dodoma.
Aliyekuwa Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye leo amekabidhi rasmi ofisi kwa Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe aliyeteuliwa hivi karibuni kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Katika makabidhiano hayo yaliyohudhuriwa na watendaji wakuu wa Wizara, Mhe. Mwakyembe ameahidi kuwa licha ya kukabidhiwa ofisi, anaamini kuwa Mhe. Nnauye bado ni mdau mkubwa wa sekta za Wizara na kuwa anategemea kuendelea kupata ushirikiano kutoka kwake.
Aidha Waziri Mwakyembe ameahidi kuendeleza yote mazuri yaliyo anzishwa na Nnauye katika kuimarisha ufanisi wa Wizara na kuhakikisha inakuwa ni moja ya Wizara za mifano nchini. Amesisitiza kuwa katika kipindi kifupi alichokaa Wizarani, Mhe. Nnauye alianzisha mabadiliko makubwa na watu wameanza kuifahamu vizuri Wizara.
Kwa upande wake Nnauye amemshukuru Rais John Pombe Magufuli kwa kumuamini na kumpa dhamana kubwa ya kusimamia Wizara kwa kipindi cha miezi 15 huku akiwa ndio kwanza amekuwa mbunge katika awamu yake ya kwanza. Aidha Nnauye ameahidi kuendela kushirikiana na Wizara kwa ukaribu kwani ni kweli yeye ni mdau mkubwa wa sekta za wizara hii.
Heshima aliyonipa Rais ni kubwa mno na nitaendelea kumuunga mkono katika dhamira yake njema ya kuleta mageuzi nchini,”  Nnauye. Aidha alisisitiza kuwa, tofauti na maneno ya mitandaoni, yeye atabaki kuwa mtiifu kwa Rais, Serikali na chama chake.

       

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search