KAMA TAYARI AU BADO HUJAMILIKI ONLINE PLATFORM, AU NI MDAU WA SOCIA MEDIA BASI HAYA YANAKUHUSU !!!

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amekemea vikali tabia iliyojengeka na inayokuwa kwa kasi miongoni wa watanzania ya kushabikia mambo yanayoweza kuhatarisha usalama wa nchi na kuandika vitu vya uongo kupitia 'social media'. Ameyasema hayo wakati wa hafla ya kuwaapisha viongozi wapya aliowateua Ikulu jijini dar es Salaam.
zifuatazo ni baadhi ya nukuu ambazo Tanzania Mpya Matukio imezinasa mchana huu wakati Dkt. Magufuli akishusha lawama hizo:


"Jana nimesoma kwenye mitandao ya kijamii kuwa eti Mwakyembe hawezi kuja kuapishwa, na mimi nilikuwa nasubiri asifike nione. ''Sasa si huyu hapa amefika"

Ameongeza kuwa..... "Jana kuna mwingine kapost Kinana kuongea na waandishi wa habari kesho, wakati ukweli Kinana nimemtuma India Kwa siku kumi na mbili"

Akamalizia kwa kuonya wamiliki wa vyombo vya habari kwa tabia yao ya kuzipa kipaumbele habari mbaya-mbaya tu zinazolichafua Taifa:  " kwa mfano kuna Tv hapa habari za migogoro ya wafugaji ndio wanazipa nafasi kubwa zaidi,... amesema hayupo tayari kuvumilia hayo mambo.

Pia hakuacha kushangaa magazeti ya leo kujaza mbele picha ya mtu mmoja, na hata kurasa za ndani kujaza habari hiyo hiyo.... na kumemwambia Mwakyembe akasimamie kwa umakini hasa tasnia ya habari,... na kutanabahisha kuwa hayupo tayari kuona nchi ikichezewa.. alimaliza Dkt. Magufuli.

Waziri Mwakiembe akiwasili ofisi za Idara ya Habari Maelezo mara baada ya kuhudhuria hafla ya kuapishwa kwake Ikulu jijini dar es Salaam, leo.


Nimekuwekea video na picha hapa usipite bila kubofya...


Na mwandishi maalum: Tanzinia Mpya Matukio


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search