KAMATI YA NAPE DHIDI YA MAKONDA: WADAU WAIBUKA NA 'RIPOTI KINZANI' NA USHAURI !

NIMEKUWEKEA HAPA JINSI WADAU WALIVYOHOJI VIPENGELE 8 VIKUU KATIKA RIPOTI….


Moja ya maswali ya kitasnia kwa Mhe waziri ni hili la ukakasi wa Members wake wa kamati:

1. Mmoja wa wajumbe ni mhariri mtendaji wa gazeti ambalo kabla ripoti hii liliweka hadharani kilichopo, je huyu atakuwa na uhalali wa kuhojiana na mtuhumiwa ?

2. Mjumbe mwengine ni mhariri kiongozi wa Gazeti ambalo mmiliki wake ambae hana mahusiano mazuri na mtuhumiwa, je huyu mjumbe huyu nae ana uhalali wa kuhojiana na mtuhumiwa?

3. Iweje aunde kamati ambayo idadi kubwa ya wajumbe wana utaalamu wa taaluma ya print media yaani magazeti, wakati tukio limetokea kwenye kituo cha radio na Luninga? Hapa kuna masuala ya broadcasting ethics na print ethics, je kanuni za kuingia news room ndio hizo za kuingia studio ya tv au chumba cha kurushia matangazo tx?

4. Mjumbe kutoka tcra anasimama kama regulator au kama nani? kwani hilo jambo linahusiana na regulator ?

5. Suala la uvamizi hilo ni suala linalohusiana na jinai haoni haja ya kuongeza wajumbe kama polisi au usalama wa taifa?

6. Mhe. mkuu wa mkoa anasimamiwa na TAMISEMI wakuu wake wana taarifa za mfanyakazi wao kuhojiwa na Kamati?

7. Kituo kinatchotajwa kuvamiwa ni kituo binafsi, na tume ina watu wengi kutoka vyombo binafsi ambao kimaslahi wana crush of interest na serikali katika baadhi ya mambo je wajumbe watakuwa huru kumuhoji Mhe makonda bila mihemuko?

8. Tayari waziri alionyesha kukerwa na tukio hilo, ameshatoa muhemko wake, je anapounda tune ambayo iko chini ya msaidizi wake kikazi haoni hapo kuna suala litaleta ukakasi?

Baada ya maswali ni Ushauri

1. Mhe waziri haoni hili jambo angelipeleka kwenye mamlaka zingine mfano jeshi la polisi, au angelipeleka TCRA au baraza la habari na kuwaomba wao kama watu huru walifanyie kazi kwa kuwa hawana mwingiliano wa moja kwa moja na hili suala?

2. Mhe Nape haoni kuna haja ya kuongeza idadi ya wajumbe huru kutoa vyuo vya kitaalumu mfano SAUT?IJMC?
Pia ofisi ya mwanasheria mkuu?

Najua hadidu rejea kuu ya kamati ni kuhoji, ila likiwekwa vizuri ili kupata mahojiano mazuri yenye maswali magumu huenda kamati ikawa BORA zaidi.

Ni maoni yangu mimi kama mwanahabari ambae napenda kujua zaidi katika sakata hili.
Source: Jamii forum.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search