1. Waziri Nape amesema ripoti aliyoipokea ataiwasilisha kwenye mamlaka za juu ili wao waone ni hatua gani wanaweza kuchukua kwa RC Makonda.
2. Kamati iliyoundwa na Waziri Nape kuchunguza sakata la kuvamiwa Clouds imesema kuwa RC Makonda alichagua kwa hiari kutokufanya mahojiano nao.
3. Tulifanya mahojiano na wafanyakazi 14 wa kituo cha Clouds.., Tulifanya jitihada za kumtafuta Mkuu wa Mkoa, tulimpigia simu lakini hakupokea.
4. Hata tulipofika katika ofisi yake, aliondoka kupitia mlango wa nyuma.., Baada ya kushindwa kuonana naye, tukajiridhisha kuwa amechagua mwenyewe kutotumia fursa ya kuhojiwa
5. Kamati imejiridhisha kuwa ni kweli RC Makonda alivamia kituo cha Clouds ambapo alikwenda kwa gari aliyokuwa akiendesha mwenyewe.
6. Chanzo cha uvamizi ni RC Makonda kutaka kurushwa kwa kipindi alichohojiwa mwanamke anayedaiwa kuzaa na Askofu Gwajima.
7. Kamati imethibitisha kuwa Makonda na Askari aliokuwa nao waliingia mpaka kwenye ofisi za kurushia matangazo kinyume na sheria.
8. Kamati imejiridhisha pia kuwa palikuwa na vitisho kwa walinzi na wafanyakazi kwa kutumia askari wenye silaha, Miongoni mwa vitisho ni kuwalazimisha kurusha kipindi vinginevyo angewaingiza kwenye tuhuma za dawa za kulevya
9. Kamati imethibitisha Makonda na Askari waliovamia Clouds waliwatisha watangazaji kuwafunga miezi sita bila kuwapeleka mahakamani na kutuhumiwa kwa dawa za kulevya.
10. Kutokana na vitisho hivyo, kipindi cha SHILAWADU kwa siku hiyo hakikufungwa kama utaratibu wa kipindi unavyotakiwa sababu ya vitisho.
11. Makonda aliwatishia wafanyakazi wa Clouds kuwa yote yaliyotokea yabaki ndani ya Clouds na wakitoa nje ya hapo watamkoma.
12. Kamati imejiridhisha kuwa Makonda alijivisha kazi ya uhariri wa vipindi kitu ambacho ni kinyume na sheria..., kamati imejiridhisha kuwa Mkuu wa Mkoa aliingilia taratibu za uhariri kwa kulazimisha habari anayoitaka iruke
13. Makonda kushinikiza kipindi ambacho hakija-'balance' kurushwa hewani, ni kuwawataka wafanyakazi wa Clouds k
No comments:
Post a Comment