MAGUFULI AWAPA ULAJI MADAKTARI 500, KWENDA KENYA KUFANYAKAZI KWA MKATABA MAALUM!!
WIZARA YAWEKA HADHARANI; WENYE VIGEZO WATAKIWA KUOMBA...
Kutoka na mgomo wa madaktari nchini Kenya, Rais Uhuru Kenyata ameiomba Serikali ya Tanzania kumsaidia Madaktari ambao wanafanya chini ya mkataba wa miaka mawili nchini huko.
Kutokana na ombi hilo,Serikali Tanzania inatarajia kupeleka madaktari 500 nchini Kenya ifikapo Aprili mwaka huu, ikiwa ni kukubali ombi la Rais Uhuru Kenyatta.
Madaktari hao watakaopatiwa ajira ya mkataba wa miaka miwili, ni wale ambao hawapo katika mfumo wowote wa ajira serikalini lakini wenye vigezo stahiki.
Akizungumza kwenye mkutano na vyombo vya habari leo, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema Rais John Magufuli amepokea ombi hilo huku akiwataka wenye vigezo kuhakikisha wanatuma maombi yao kabla ya Machi 27.
"Daktari anatakiwa asiwe ameajiriwa katika hospitali ya Umma, awe amepata mafunzo kwa vitendo na pia awe amesajiliwa na Baraza la Madaktari Tanzania," alisema Ummy Mwalimu.
Source: tanzaniampyamatukio blog




No comments:
Post a Comment