MAKALA: AFYA YA JAMII - MADHARA YANAYOSABABISHWA NA ULAJI MWINGI WA SUKARI

PITIA MAKALA HII YA UCHAMBUZI UWEZE KUZIJUA NJIA NNE (4) KUU ZA KUPUNGUZA ULAJI MWINGI WA SUKARI

Tunafahamu kuwa ulaji wa sukari kupita kiasi unahusishwa na kuongezeka kwa unene, uzito kupita kiasi, ugonjwa wa kisukari cha ukubwani (aina ya pili), magonjwa ya moyo, baadhi ya saratani, kuoza kwa meno na ugonjwa wa ini.
Mfumo wa mwili wa binadamu unaothiriwa na ulaji mwingi wa sukari!
Hata hivyo katika nchi zinazoendelea kama Tanzania, siyo rahisi kufanya tafiti zinazoonyesha kiasi cha sukari anacho kula mtu kwa siku.

Lakini baadhi ya tafiti za miaka ya 2008-2009 zinaonyesha kuwa nchini ya Marekani mtu mzima kwa wastani anakula sukari vijiko vya chai 22 kutoka katika vyakula vilivyosindikwa kiwandani.
Kwa mujibu wa Taasisi ya Kimarekani ya Mambo ya Moyo (Aha), kwa watu wazima, wanawake, matumizi yao ya sukari inayotokana na vyakula vilivyosindikwa kiwandani, yasizidi vijiko sita vya chai kwa siku.

Huku kwa upande wa wanaume wasizidishe vijiko tisa kwa siku na kwamba wataalamu wanabainisha kuwa kila gramu nne za sukari ni sawa na sukari iliyojaa katika kijiko kimoja cha chai.
Wataalamu hao wanasisistiza kuwa maelezo katika vyakula vilivyosindikwa viwandani yawe kwenye kifungashio cha bidhaa.

Sukari ni chanzo muhimu cha nishati mwilini.
Watu wanasema bila sukari hakuna uhai, hivyo kuacha kabisa kula vyakula vya wanga na vyenye sukari unaweza kusababisha mwili kuwa na kiwango kidogo sana cha sukari na kuathiri ufanyaji kazi wa ubongo na viungo vingine.
Na kwamba hali kama hiyo ikiendelea, mtu anaweza kuishiwa nguvu na kupoteza fahamu na wakati mwingine kusababisha kifo kwani sukari nyingi ni sumu na inadhuru afya.
Ulaji wa sukari kupita kiasi unahusishwa na kuongezeka kwa unene, uzito kupita kiasi, ugonjwa wa kisukari cha ukubwani (aina ya pili), magonjwa ya moyo, baadhi ya saratani, kuoza kwa meno na ugonjwa wa ini.

Njia 4 kuu za kupunguza ulaji wa sukari:
Miongoni mwa njia hizo ni kwanza ni:
·       kuwa na ufahamu wa kutosha kuhusu hatari ya kiafya inayotokana na ulaji wa sukari nyingi. Matumizi hayo ya sukari yanamfanya mtu awe anapenda sukari mfano kwa wale walio athiriwa na dawa za kulevya.
·       Njia ya pili ni kubainisha chanzo kikubwa cha sukari katika vyakula na vinywaji unavyotumia kila siku, hapa unatakiwa kupunguza unywaji wa juisi za viwandani na vitu vingine ambavyo ni vitamu.
·       Vile vile, jambo jingine ni kupunguza matumizi ya ulaji wa vyakula vyenye sukari kama vile chai yenye sukari nyingi, keki, mikate ya kumimina au visheti.

Tende: ni moja chakula mbadala vinavyosaidia kupunguza ongezeko la sukari nying mwilini

Unaweza chunguza pia kama una kawaida ya kula vyakula vyenye kiwango kikubwa cha sukari ama wanga. Mfano kilichotokana na unga wa mahindi yaliyokobolewa.
Baada ya kujua chanzo kikuu, weka mpango wa kupunguza ulaji wa vyakula hivyo. 
·       Kama unaweka vijiko vinne vya sukari katika chai au kahawa, punguza hatua kila wiki kijiko kimoja na hiyo itapunguza tatizo hilo.

Hata hivyo baada ya wiki tatu utakuwa unakunywa chai na kuweka kijiko kimoja cha sukari.
Hivyo kama unakunywa soda kila siku chupa tatu, asubuhi, mchana na jioni sasa unashauriwa kupunguza iwe chupa moja kila siku na baada ya wiki moja punguza mpaka uweze kunywa chupa moja ya soda kila baada ya siku mbili na baadaye uweze kunywa soda chupa mbili kwa wiki.

Sukari ya viwandani 

Baada ya hapo unaweza kujitathimini sasa kama unaweza kuishia hapo au kuacha kabisa kunywa vinywaji hivyo na kutumia vinywaji halisi kwa kusaga matunda bila kuweka sukari.
Mwisho.

Makala hii ya jamii imekujia kwa msaada wa mitandao mbali mbali inayojishughulisha na Afaya ya jamii na kuhaririwa na Tanzania Mpya Matukio.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search