7-1 wa Barcelona umeishusha daraja Osasuna, Real akipata ushindi wa 6-2

Baada ya kumalizika kwa mchezo wa El Clasico April 23 kati ya Real Madrid waliyowakaribisha wapinzani wao wa jadi FC Barcelona katika uwanja wao wa Santiago Bernabeu na Madrid kupoteza kwa magoli 3-2, usiku wa April 26 Real Madrid walikuwa ugenini kuwakabili Deportivo wakati Barcelona wakiikaribisha Osasuna katika uwanja wa Nou Camp.

Barcelona akiwa nyumbani amefanikiwa kupata ushindi wa magoli 7-1 dhidi ya Osasuna na kuishusha daraja timu kutokana na Leganes wamepata ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Las Palmas, hivyo rasmi Osasuna wanacheza michezo ya kukamilisha ratiba LaLiga na wanasubiri kucheza Segunda msimu ujao.

Javier Mascherano akifurahia goli lake la kwanza katika maisha yake Barcelona toka alipojiunga nayo 2010 akitokea Liverpool ya England amecheza jumla ya mechi 319

Real Madrid wao wakiwa ugenini dhidi ya Deportivo La Coruna katika uwanja wa Riazor wamefanikiwa kupata ushindi wa magoli 6-2, licha ya kuwakosa wachezaji wao nyota kama Toni Kroos na Ronaldo waliyopumzishwa, nahodha wao Sergio Ramos anayetumikia adhabu ya kadi nyekundu ya El Clasico na Gareth Bale ambaye atakuwa nje ya uwanja kwa wiki tatu kwa kuwa na majeruhi.

Msimamo wa LaLiga baada ya matokeo ya mechi za April 26 2017
credit: millard ayo

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search