BREAKING NEWS!! MUHIMBILI WAENDESHA UPASUAJI WA KIHISTORIA


Mojawapo ya Majengo makuu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili

Hospitali ya Taifa Muhimbili leo imeanza kufanya upasuaji wa kihistoria wa kuondoa uvimbe 'fibroid' kwa wanawake ambao umefanyika kwa njia ya matundu madogo (laparoscopic Surgery).

Upasuaji huo unaofanyika katika chumba kikuu cha upasuaji, unaenda sambamba na mafunzo kwa vitendo kwa madaktari zaidi ya 30 ambao wanafuatilia moja kwa moja kwa njia ya runinga wakiwa chumba cha mkutano. Daktari bingwa wa uzazi na magonjwa ya wanawake Vicent Tarimo alisema upasuaji wa aina hiyo kwa njia ya kawaida huchukua takribani saa moja na nusu mpaka mawili, lakini kwa njia hiyo ya kisasa wamefanikiwa kumtibu mwanamke aliyekuwa na uvimbe kwenye mirija ya uzazi kwa saa moja.

"Zaidi ya wanawake 15 watanufaika na upasuaji huu na wengi wamekuwa na tatizo la uvimbe sehemu mbalimbali kuzunguka kizazi," alisema.

Na Mwandishi wetu.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search