#Marekani yajishusha; yesema iko tayari kwa mazungumzo na Korea Kaskazini !

Rex Tillerson (kulia) na balozi wa Marekani kwenye UN Nikki Haley

Marekani iko tayari kwa mazungumzo na Korea Kaskazini yenye lengo la kuondoa zana za nuklia kutoka eneo hilo, kwa mjibu wa waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani Rex Tillerson.
Lakini amesema kuwa Marekani itatumia nguvu za kijeshi ikiwa itahitajika.
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa China, mshirika mkubwa wa Korea Kaskazini, anasema makubaliano ya amani ndio njia pekee.
Bwana Tillerson aliliambia baraza la ulinza la Umoja wa Mataifa kuwa tisho la Korea Kaskazini la kushambulia majirani zake na zana za nuklia.
Maelfu ya wanajeshi wa Marekani wako nchi majirani wa Korea Kaskazini ikiwemo Korea Kusini na Japan.

Tillerson amezitaka nchi wachama wa Umoja wa Mataifa kuiwekea Korea Kaskazini vikwazo na kupunguza uhusiano wao wa kidiplomasia na nchi hiyo.
"Kwa miaka kadha Korea Kaskazini imekuwa ikiendesha kwa nguvu mpango huu hatari."

"Ni wakati wetu kuchukua hatua na kudhibiti hali," Tisho la Korea Kaskazini la kufanya shambulizi la nuklia dhidi ya Korea Kusini au Japan ni la kuwezekana, na ni muda tu kabla ya Korea Kaskazini kufanikiwa kupata uwezo wa kushambulia Marekani." alisema Tillerson.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search