FLORA MBASHA AMTAJA MWANAUME ATAKAYEFUNGA NAE NDOA WIKI IJAYO

maxresdefault

     Muimbaji nyota wa muziki wa Injili nchini, Madame Flora (Flora Mbasha zamani), Jumapili ya wiki ijayo anatarajia kufunga ndoa na mume wake mtarajiwa Daudi Kusekwa katika bustani za hoteli ya Rock Beach jijini Mwanza.
    Madame Flora ameliambia Swaggaz kuwa ndoa hiyo itaambatana na uzinduzi wa albamu yake mpya inayoitwa Wakati Wake pamoja na kitabu alichokipachika jina la Siri za Flora Mbasha.
    “Ndoa itafungwa asubuhi na jioni kutakuwa na sherehe ya harusi, utambulisho wa albamu yangu mpya pamoja na kitabu, watu wote wanakaribishwa kadi zimebaki chache tu kutokana na idadi ya ambayo imepangwa na kamati,” alisema Flora.
    Awali. Flora alikuwa ameolewa na mwanamuziki mwenzake wa nyimbo za Injili Emmanuel Mbasha lakini walitengana.

    Swahili times

    About Author Matukio360

    Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

    No comments:

    Post a Comment

    Leo leo Plus

    Start typing and press Enter to search