HAJI MANARA AFUNGUKA MAZITO YA HUKUMU YA TFF.. ASEMA ATAPAMBANIA HAKI KWA VIWANGO VYA JUU !!
MSEMAJI MKUU wa Simba aliyefungiwa, Haji Sunday Manara
amefunguka mazito kuhusu hukumu iliyotolewa dhidi yake akidai kwamba
hakutendewa haki.
Akiongea kupitia ukurasa wake wa Instagram baada ya kurejea
kutoka katika majukumu ya kifamilia Zanzibar ameelezea mkasa mzima na kwamba
hakuona uharaka wa TFF kung’ang’ania kutoa maamuzi licha ya mwajiri wake
kuiandikia barua TFF ya kuomba kusogeza mbele kikao mpaka siku ya J’nne ili
apewe nafasi ya kusikilizwa.
“Mimi si mtu ninayeamini uonevu na si mtu ninayeweza
kunyamaza nikiona haki inaporwa…” alisema Haji.
Akielezea kadhia nzima ya maamuzi ya TFF Haji alisema…
Mimi si mtu mwenye moyo dhaifu wa kuogopa kukosoa pale
panapopaswa kurekebishwa, na always nitabaki hivyo…”,
Haji amesema kuwa siku alipopata taarifa ya kuitwa TFF, alikuwa Zanzibar kwa maswala ya kifamilia na
ndipo mwajiri wake alivyoandika barua kuomba kusogezwa mbele kwa kikao hicho
jambo ambalo TFF ilipuuzia.
“Barua iliwafikia na binafsi nikaongea na Afred Lucas msemaji
wao na akanijibu ameipokea yeye na imegongwa muhuri na Katibu Mkuu wa TFF ameshaipata”
Ni uharaka upi iliyonao TFF wa kushindwa kunipa nafasi ya
kunisikiliza?, alisema Haji na kuongeza… Natural justice nchi hii haitambuliki,..
endapo wahaini na wauaji hupewa nafasi ya kusikilizwa iweje kwangu ninaepiga
kelele kutetea haki ya mwajiri wangu ? aliuliza Haji.
“Nimejiuliza, hivi ni kaka yangu huyu Msemwa aliyesoma hii
hukumu?... ukweli ni kwamba nimemuona
kwa Millard Ayo, anasoma hukumu iliyo kinyume cha hati ya mashtaka,…”
“Ni aina ya hukumu katili zaidi kwa viwango vya mpira wetu,
ila nawaambia TFF Haji hajawahi kuwa dhaifu wa moyo, anaweza kuwa dhaifu wa
kiwiliwili, lakini nina moyo wa Simba,… nitapambana kutetea haki yangu na ya mwajiri
wangu kwa viwango... alimaliza.
Je, Haji kaonewa au hajaonewa?… tupe maoni yako.




No comments:
Post a Comment