PART 1: NJIA 25 ZA KUONDOA AU KUPUNGUZA MAFUTA TUMBONI KWA WANAWAKE
Wanawake wengi miaka ya karibuni wanakabiliwa na tatizo linalofanana na kitambi kwa upande wa wanaume. Hivyo ingekuwa ni wanaume tungesema ni kitambi ambalo nalo ni tatizo kubwa miongoni mwa wanaume wengi nyakati za sasa.
Kinachowasumbuwa wanawake siyo kitambi tunasema ni
mlundikano wa mafuta sehemu ya chini ya tumbo na tumbo kwa ujumla kufikia hali
kuonekana kama ana tumbo kubwa au kuhisi labda ni ujauzito kumbe ni mafuta tu
mengi.
Kwa ujumla ni vigumu sana kupunguza tumbo la namna hii,
hivyo kwenye post hii pamoja na mengine tutaona pia visababishi vya tatizo
lenyewe, dawa za asili zinazoweza kuondoa tatizo hilo na aina ya maisha
unayotakiwa kuishi ili ufanikiwe kirahisi zaidi bila kukuachia madhara mengine
yoyote.
Nini kinasababisha tumbo kwa kina mama:
*Vyakula feki (Junk food)
*Kutumia vyakula vya wanga kupita kiasi
*Kutokunywa maji ya kutosha kila siku
*Kula chakula kizito muda mchache kabla ya kwenda kulala
*Kukaa masaa mengi kwenye kiti
*Kutokujishughulisha na mazoezi
*Mfadhaiko (stress)
*Kula wali kila siku
*Ugali wa sembe
*Kula vyakula vinavyopikwa katikati ya mafuta mengi (chipsi,
maandazi, nk)
Vyakula 25 vinavyoondoa mafuta kwenye tumbo kwa wanawake
1. ASALI NA LIMAU
Chukua asali kijiko kikubwa kimoja cha chakula na majimaji
ya limau vijiko vikubwa viwili, changanya hivi viwili ndani ya glasi moja (robo
lita) ya maji ya uvuguvugu na unywe yote mara tu ukiamka asubuhi.
Tumia kwa wiki 3 hivi mpaka mwezi mmoja na hutachelewa kuona
tofauti.
2. MAJI YA UVUGUVUGU
Kunywa maji ya uvuguvugu kama lita 1 hivi wakati tumbo
likiwa tupu hasa asubuhi ukiamka tu. Hii inasaidia kusafisha mwili na kuondoa
mafuta yasiyohitajika.
3. NYANYA
Kula nyanya ambazo hazijapikwa pia inasaidia kupunguza tumbo
kwa kina mama, hivyo kula kachumbali ya kutosha kila siku ya nyanya peke yake
na utaona mabadiliko.
4. TANGAWIZI
Chemsha chai ya tangawizi, ipua na usubiri ipowe kidogo,
ongeza asali mbichi kidogo na pilipili manga kidogo ya unga. Pata kikombe
kimoja cha chai hii kila siku asubuhi mapema ukiamka tu. Asali inasaidia
kuyeyusha mafuta wakati pilipili itauongezea nguvu mfumo wa mmeng'enyo wa
chakula.
5. SIKI YA TUFAA
Siki ya tufaa (apple cider vinegar) inasaidia kupunguza njaa
na kukufanya ujisikie umeshiba kwa kipindi kirefu. Kunywa kijiko kikubwa kimoja
cha siki ya tufaa mara 1 kwa siku kila siku wakati unakula chakula cha usiku.
Kazi nyingine ya hii siki ni kuweka sawa damu sukari mwilini hivyo ni nzuri pia
kwa wenye kisukari.
6. MAJANI YA BIZARI
Majani ya bizari husaidia kuondoa sumu na takatka nyingine
mwilini kitu ambacho moja kwa moja hupelekea mlundikano mdogo wa mafuta katika
tumbo. Kunywa chai ya majani ya bizari kila siku asubuhi, ukikosa majani
unaweza kutumia hata unga wake.
8. ILIKI
Iliki hufanya kazi ya kuongeza nguvu katika mfumo wa
mmeng'enyo wa chakula na ni dawa nzuri sana ya kuondoa sumu na takataka
nyingine mwilini. Iliki pia hutumika katika kupunguza uzito. Tengeneza chai
yenye iliki kila siku ndani yake, pia ni kiungo karibu kwa vyakula vingi hivyo
hakikisha unaiweka katika kila chakula unachopika kwa matokeo mazuri zaidi.
9. MDALASINI
Mdalasini hufanya kazi ya kuchoma mafuta mwilini. Chukua kijiko
kidogo kimoja cha mdalasini ya unga na uweke ndani ya glasi 1 ya maji ya moto
na uache kwa dakika 5 hivi. Ongeza kijiko kidogo kimoja cha asali mbichi ndani
yake na ukoroge vizuri, kisha unywe huo mchanganyiko wote asubuhi ukiamka tu.
10. JUISI YA LIMAU
Kunywa maji ya limau au juisi ya limau kila mara
kutakusaidia kuondoa mafuta tumboni kwa haraka sana. Ongeza majimaji ya limau
vijiko vikubwa viwili ndani ya glasi 1 ya maji na uongeze punje 1 ya chumvi ya
mawe, koroga vizuri na unywe asubuhi ukiamka tu kila siku.
itaendelea...




No comments:
Post a Comment