KAMA ULIPITWA NA HII: MAALIM SEIF AONGELEA YA LIPUMBA KUVAMIA MKUTANO WA CHAMA

Jana April 9 2017 Maalim Seif amesema Dola imekuwa ikitumia njama na mbinu chafu ilikuhujumu chama cha CUF kwa kumtumia Lipumba baada ya kumkaribisha Ikulu na kumtumia kushawishi chama hicho kishiriki marudio ya uchaguzi wa march 20 2016.
Akizungumza na waandishi wa habari aliyaongea haya…>>>Njama hizi zilianza mara baada ya kibaraka Ibrahim Lipumba kukaribishwa Ikulu mapema mwaka jana,nyote mnakumbuka sinema ya Lipumba kwanza alitumiwa kutushawishi kushiriki uchaguzi haramu wa marudio wa March 20 2016 huku akiniambia mimi binafsi kuwa nikubali kwani angalau nitaweza kuendelea kuwa makamu wa Rais wa kwanza wa Zanzibar’- Maalim Seif


Source: Millard Ayo



About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search