KOMBORA LA KOREA KASKAZINI LASHINDWA KUPAA!
Korea Kaskazini imejaribu kufyatua kombora moja lakini likakosa kupaa angani, siku moja tu baada ya kuonya Marekani kuwa haiogopi vitisho vyake vya kivita.
Jeshi la Marekani lilisema kuwa kombora hilo lililipuka sekunde chache baada ya kufyatuliwa katika ufuo wa Mashariki wa Korea Kaskazini.
Afisa mmoja wa Marekani alisema kuna uwezekano mkubwa kuwa kombora hilo halikuwa la masafa marefu linaloweza kutoka bara moja hadi jingine.
Rais Trump alifahamishwa juu ya jaribio hilo lililofanywa masaa machache kabla ya Makamu wa Rais Mike Pence kuwasili Korea Kusini, kwa mashauri kuhusiana na Pyongyang na mipango yake ya makombora ya kinyukilia.
Hali ya uhasama kati ya Korea Kaskazini na Marekani imekuwa ikipanda, huku kila upande ukijigamba jinsi utakavyoweza kuchafua upande mwingine.
Mnamo Ijumaa Uchina iliitisha mkutano unaonuia kutuliza uhasama huo. 
Kombora la Korea Kaskazini lashindwa kupaa siku moja baada ya maonyesho ya zana na kijeshiHaki miliki ya pichaREUTER

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search