Video: Diamond Platnumz.. Atua Kigali, aahidi 'kuwashika' Wanyarwanda !! #share

Msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amewasili nchini Rwanda jana jioni tayari kwa kuwakonga nyoyo mashabiki wake nchini humo kwenye tamasha la Fiesta wikiendi hii na kuahidi kuwa wajiandae kuja na vitambaa vya kufutia machozi.



Akiongea na waandishi wa habari mapema jana baada ya kushuka Airport jijini Kigali amesema Show yake ya Rwanda itakuwa ni ya kipekee kwani ameenda na Bendi na timu kubwa hivyo mashabiki wakae mkao wa kula na waandae leso kabisa za kufutia machozi.

“Nafikiri waje na viatu vitakavyowawezesha kucheza kwa sababu tutakuwa tunaimba na kucheza pamoja kama unavyojua mimi nina nyimbo nyingi za kucheza,” amesema Diamond Platnumz huku akiwasisitiza kuja na leso za kufutia machozi


“Waje na leso pia kwa sababu tutakuwa na nyimbo zingine za huzuni kwa hiyo watalia,” amesema Diamond Platnumz.

Diamond Platnumz anatarajiwa kuondoka leo jioni kwenda Goma nchini DR Congo na baadae kurejea Rwanda Julai 2 kutumbuiza kwenye tamasha hilo ambalo litafanyika nje kidogo ya jiji la Kigali... Bongo5.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search