MH. WAZIRI ANGELA KAIRUKI: KIPIMO CHA VIONGOZI WA KISIASA NI KUJUA KUSOMA NA KUANDIKA HIVYO HIVYO HAWAKUHUSIKA NA ZOEZI HILI LA UHAKIKI WA KUBAINI VYETI FEKI !
Akiwasilisha taarifu fupi ya zoezi la uhakiki waziri Kairuki alikuwa na haya ya kusema:
"Zoezi hili la uhakiki lilihusisha watumishi wa umma
pekee wakiwemo Makatibu wakuu na watendaji wengine. Watumishi hawa wanatakiwa
kuwa na sifa za kutumikia nafasi zao.
Zoezi hili halikuhusisha Viongozi wa Kisiasa wakiwemo
Mawaziri, Wabunge, Wakuu wa Mikoa/Wilaya na Madiwani ambao wanatakiwa kujua
kusoma na kuandika tu!
Ripoti hii inaonesha kuwa tayari watumishi wa Umma
400035 wamehakikiwa.
Matokeo ya uhakiki yamegawanyika kwenye makundi manne:
1. 376969 sawa na 94.23% wana vyeti halali. Baraza
limehakikisha kuwa magamba ya vyeti vilivyohakikiwa vilitolewa na NECTA na
taarifa zao zinaendana na zilizopo kwenye vyeti.
2. 9932 sawa na 2.4% wamebainika kuwa na vyeti vya kughushi.
Vyeti vyao havifanani na vinavyotolewa na NECTA.
3. Vyeti 1538 vinatumika na zaidi ya mtumishi mmoja
ambayo ni sawa na 0.3% ya vyeti vilivyohakikiwa. Hawa tunasema wana vyeti
vyenye utata.
4. 11569 waliwasilisha vyeti pungufu. Hawa
waliambatanisha vyeti vya utaalamu kama udaktari au ualimu pekee bila vyeti vya
kidato cha nne wala cha sita.
Kwa mujibu wa kanuni ya adhabu, adhabu ya mtu
aliyefanya kosa la kughushi cheti ni kifungo Jela miaka 7.
Waziri Kairuki amekabidhi ripoti na boksi lenye majina
ya watumishi na taarifa zao kamili kama wako wapi na wanapatikana wapi.
Rais anatoa kitabu na kusoma jina la mtumishi mmoja
" Abdallah Chanja" na kusema mengine atayasoma kwa wakati wake.
Source: JF
No comments:
Post a Comment