MITAALA YETU: TWAWEZA WAZINDUA RIPOTI YA 'UWEZO WA WANANFUNZI DARASANI' KIINGEREZA KAMA SOMO LA KUFUNDISHIA LINA 'CHANGAMOTO' NYINGI.

Taasisi Twaweza wamezindua ripoti ya Tathmini ya 6 ya matokeo ya kujifunza nchini ya #Uwezo huko Dodoma. Tathmini hiyo imebainisha matokeo ya kujifunza pamoja na mazingira ya kujifunzia nchini Tanzania kutokana na utafiti ya mwaka 2015.

WhatsApp Image 2017-04-10 at 14.54.14.jpeg 

Katika moja ya matokeo ni kuhusu uwezo wa kusoma kiingereza katika Shule za Msingi. Uwezo huu umepimwa kwa darasa la 3 na la 7 kwa kutumia mtaala wa darasa la 2 kwa wanafunzi wote.

13% (Mmoja kati ya Kumi) tu ya wanafunzi wa darasa la 3 waliweza kusoma hadithi ya kiingereza ya darasa la 2. Kama tu hiyo haitoshi 52% ya Darasa la 7 walishindwa kusoma hadithi ya kiingereza ya Darasa la 2.

Screenshot from 2017-04-10 12-46-30.png 

Je Matokeo haya yanaashiria nini? Je ni ubovu wa mitaala ya kiingereza? Je ni ugumu wa lugha hii? Je walimu wanachukuliaje hali hii kwa wanafunzi wao?

Source: Jamii forum

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search