MWANAMUZIKI 'ROMA MKATOLIKI' AKAMATWA AKIWA STUDIO !


Mwanamuziki Rhymes Of Magic Attraction maarufu Roma Mkatoliki amekamtwa usiku wa kuamkia leo akiwa katika Studio za kutayarishia muziki za Tongwe Records jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na mwanamuziki mkongwe, Joseph Haule maarufu Professor Jay, Roma Mkatoliki akiwa pamoja na mwanamuziki mwingine, Moni na mfanyakazi mmoja wa studio hiyo walikamatwa na watu wasiojulikana jana saa moja jioni na kupelekwa eneo lisilojulikana.
Mbali na wasanii hao kukamatwa, watu hao pia walichukua tarakilishi (computer) na runinga mali ya studio hiyo. Aidha, watu hawakueleza sababu za kutekeleza tukio hilo.
“Nimestushwa sana kusikia kuwa kuna watu wamevamia studio za TONGWE RECORDS majira ya saa moja usiku na wamemchukua ROMA @roma2030 , MONI @moni_centrozone na kijana wa kazi,” aliandika Professor Jay kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Aliendelea kuandika’ “Pia wamechukua COMPUTER ya studio na Screen (Tv) na wameondoka navyo kusikojulikana..

Mpaka sasa hatujui wamewapeleka wapi!!”

Source: swahili times


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search