NEWS ALERT !! BASHE AOMBA MWONGOZO AKILEZEA 'VITISHO' KWENYE UJUMBE ALIOTUMIWA !
![]() |
| Mbunge Hussein Bashe akiongea leo Bungeni |
Kutoka Bungeni DODOMA, leo April 10, 2017 Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe amesimama kuomba muongozo kwa Naibu Spika wa Bunge akitaka Bunge lisimamishe shughuli za kawaida na kuanza kujadili matukio ya utekaji watu yanayoendelea nchini.
Bashe amesema yeye pia ameshatumiwa ujumbe wa vitisho wakimwambia kuna watu 11 akiwemo yeye watafanyiwa vitendo vibaya popote watakapokuwa, hivyo analiomba Bunge lijadili suala hilo kwa dharula kwasababu sio sawa kukaa kimya.
>>>’Kuna watu wamenitumia jumbe za kuniambia kwamba mimi ni kati ya watu 11 ambao tupo hatarini kufanyiwa vitu vibaya na popote pale nijiangalie ninapokuwa barabarani'<<<
Mbunge wa Nzega Mjini Hussein Bashe, leo ameongelea hali ya usalama wake kufuatia kupokea ujumbe wa maneno ukimuarifu kuwa miongoni wa watu 11 waliomo kwenye orodha ya watu wanaosakwa kwa ajili ya kufanyiwa vitu vibaya...
Kupitia ukurasa wake wa twitter ambao 'matukio' uliitembelea, Bashe aliandika haya..
"Kuna watu wamenitumia ujumbe kwamba mimi ni kati ya watu 11 tuliopo hatarini kufanyiwa vitu vibaya popote pale nijiangalie. Hatuwezi kulifumbia macho jambo hili, Watanzania wanatekwa na watu wasiojulikana".
Bunge na Serikali haiwezi kulifumbia macho jambo hili la Haramu wakati Watanzania wanatekwa na watu wasiojulikana.













No comments:
Post a Comment