#PEP GUARDIOLA ANENA BAADA YA #CLAUDIO BRAVO KUPATA MAUMIVU MAKALI !

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola amesema hafahamu iwapo mlindalango wa klabu hiyo Claudio Bravo ataweza kucheza tena baada ya kuumia wakati wa mechi kati ya City na Manchester United Alhamisi.
Bravio, 34, aliondolewa uwanjani kwa machela baada ya kuumia akijaribu kuondosha mpira kutoka eneo la hatari wakati wa mechi hiyo ya Ligi ya Premia.
Willy Caballero aliingia nafasi yake.
"Bila shaka ni jeraha, labda litamuweka nje wiki kadha," alisema Guardiola,
"Sijui kama ataweza kucheza tena msimu huu."
Sare hiyo tasa, ambayo Bravo aliondoka uwanjani dakika ya 79, ilikuwa mechi yake ya sita kucheza kati ya 22 alizocheza Ligi ya Premia bila kufungwa tangu anunuliwe £15.4m kutoka Barcelona

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search