Sikiliza  Walichosema TRA kuhusu kunyang'anywa basi Serengeti Boys April 4

Siku moja baada ya kampuni ya udalali ya YONO Auction Mart ambao ni mawakala wa udalali wa mamlaka ya mapato Tanzania TRA kuinyang’anya na kuishusha katika basi timu ya taifa ya vijana chini ya umri chini ya miaka 17 Serengeti Boys wakiwa njiani kuelekea katika mualiko wa chakula cha jioni na Makamu wa Rais.
Sports Extra ya Clouds FM imempata mkurugenzi wa huduma na elimu ya mlipa kodi wa TRA Richard Kayombo aelezee kuhusiana na suala hilo, ambapo Serengeti Boys walishushwa kutokana na deni la kodi la shirikisho la soka Tanzania TFF kutolipwa hadi sasa.
“Tunasikitishwa sana na kilichotokea lakini tuliagiza kampuni iliyofanya hivyo iliachie basi hilo mara moja na walifanya hivyo na tunafanya taratibu za kinidhamu kuhusiana na tatizo hilo na tutachukuwa hatua juu ya suala hilo kulingana na mkataba wetu na kampuni husika”(source:Millard Ayo)

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search