TUNDU LISSU: NIMENUSURIKA KUPIGWA NA STEVEN WASSIRA



Source: Swahili times. Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu alinusurika kushambuliwa na aliyekuwa Mbunge wa Bunda, Steven Wassira katika moja ya vikao vya Bunge Mjini Dodoma.
Lissu aliyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano na gazeti la Mwananchi kuhusu maisha yake binafsi na mambo mbalimbali ambayo amewahi kukutana nayo, ambapo alielezea pia kesi ambazo zinamkabili, maisha ya mahabusu, familia yake, burudani anazopenda pamoja na uhusiano wake na watu mbalimbali.
Mbunge huyo alisema Wassira alitaka kumpiga baada ya maneno makali aliyomtolea bungeni wakati akichangia hoja. Miongoni mwa maneno yaliyomkwaza Wassira ni baada ya Lissu kumwambia kuwa alijiunga upinzani akidhani kuna fedha na alipogundua hakuna ndipo akakimbia kurudi CCM.
“Alichukia sana. Sasa nimetoka pale naenda chooni, nikamkuta akiwa na wabunge wengine wa CCM. Aliponiona akaanza kunifuata akiniambia kuwa atanipiga, alisema Lissu
Lissu alisema kuwa alimuona Wassira akizidi kumkaribia ambapo alikuwa akielekea kwenye kona ili ampate vizuri. “Na akikasirika anakuwa mkubwa kweli, alafu mimi mdogo. Nikawa nawaangalia wale wabunge wengine wa CCM kama wataingilia kuamua, naona hakuna anayetaka kumzuia.”
Akisimulia tukio hilo Lissu alisema, Wassira alirusha ngumi ya kwanza akaikwepa, aliporusha ya pili ikamkosa huku Wassira anazidi kusogelea, akawaza kuwa akipiga hatua nyingine moja atampiga teke, wakati anaugulia maumivu yeye atakimbia. Lakini Wassira aligeuka na kuondoka zake.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search