VIDEO: Arsenal vs Man City game imemalizika 2-2, msimamo wa EPL upo hivi
Rama Mwelondo TZA Na millardayo.com
Jumapili ya April 2 2017 game za Ligi Kuu England zilichezwa kama kawaida ila game ya Arsenaldhidi ya Man City ndio ilikuwa game inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa EPL, Arsenal walikuwa wenyeji wa Man City katika uwanja wa Emirates.
Arsenal wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani wamejikuta wakiambulia sare ya kufungana goli 2-2, magoli ya Arsenal yakifungwa na Theo Walcott dakika ya 40 baada ya Leroy Sane kuifungia Man City goli la kuongoza dakika ya 5 na Sergio Aguero akapachika goli la pili ambalo lilisawazishwa na Shkodran Mustafi dakika ya 54.
Sare ya Arsenaldhidi ya Man City inakuwa ni sare yao ya 45 toka wakutane November 11 1893 katika mchezo uliyomalizika kwa Arsenal kupata ushindi wa goli 1-0 ila Man City ilikuwa ikiitwa Ardwick wakati huo, wamekutana mara 190, Man City akishinda mara 50 na Arsenal akishinda mara 95.


About Author Matukio360
Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.
No comments:
Post a Comment