UBUNGE AFRICA MASHARIKI: 'CUF- LIPUMBA' YAPELEKA SIMANZI CHADEMA!!
Baada ya Wagombea waliopendekezwa na chadema Wenje Na Masha kupigiwa kura nyingi sana za HAPANA kuwania kuiwakilisha tanzania katika bunge la africa maahariki kumejitokeza hali ya simanzi kubwa miongoni mwa wanachama wa chama hicho chenye Wabunge wengi kutoka kambi ya Upinzani huku Mwenyekiti wa chama bwana Freeman Mbowe akitoa tamko rasmi la kutokutambua matokeo.
Mbowe ameibuka na kuongea na wanahabari na kusema kuwa wanapinga matokeo hayo, na wanajiandaa kufungua kesi mahakamani kupinga matokeo hayo, huku chama cha CUF kikipata nafasi moja pekee kutoka kambi ya Upinzani hatua inayoonekana kama ni ushindi kwa Prof. Lipumba kwa hisia kwamba Mhe. Mnyaa ni 'Lipumba wing' katika mgogoro wa madaraka unaoendelea kati ya Prof. Lipumba na Maalim Seif Sharif Hamad.
Awali msimamizi wa Uchaguzi huo akitangaza washindi alisema: Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepiga kura za kuwapitisha wawakilishi wa bunge la Afrika Mashariki ambapo wagombea saba pekee ndio waliopitishwa kwa kupigiwa kura za ndio huku sita kati yao wakitokea Chama cha mapinduzi (CCM) na mmoja Chama cha wananchi CUF huku wagombea wawili wa CHADEMA wakikosa sifa baada ya kupigiwa kura nyingi za HAPANA.
Washindi wa nafasi hizo ni kama wafuatao:
1. Fancy Nkuhi
2. Happiness Legiko
3. Maryam Ussi Yahya
4. Dkt Abdullah Makame
5. Dkt Ngwaru Maghembe
6. Alhaj Adam Kimbisa
2. Happiness Legiko
3. Maryam Ussi Yahya
4. Dkt Abdullah Makame
5. Dkt Ngwaru Maghembe
6. Alhaj Adam Kimbisa
7.Habib Mnyaa (CUF)
Source: Tanzania Mpya Matukio
No comments:
Post a Comment