VITA BADO MBICHI TFF VS HAJI SUNDAY MANARA!!
Msemaji wa Simba aliepewa adhabu Haji Manara amelalamikia kutopewa haki ya kusikilizwa na chama cha mpira nchini. Manara amedai hati ya mashtaka ya TFF imemtuhumu kwa kutaja ukabila ila haielezi hata kosa moja walilomfungia nalo kati ya matatu waliyosema anayo.
Amedai ameandikiwa hati ya mashtaka nyingine na hukumu imesomwa kivingine, amesema vita ni kubwa kuliko watu wanavyofikira, amesisitiza ni war na sio battle.
Kuhusu adhabu ya Simba ameshangazwa na TFF kuzungumzia madai yawaalikwa na kuacha hoja ya msingi ya kadi tatu za njano.
Haji ameongeza TFF imekuwa mkubwa kuliko baraza la michezo nchini(BMT) na serikali kwani imepuuza maagizo yao na amedai anaweza kuzuiwa kuzungumzia habari za Simba lakini hawezi kuzuiwa kuzungumzia mpira. Ameongeza mpira nchi hii hauendi kwani mchana wanatoa hukumu nyingine na jioni wanatoa maamuzi mengine.
Manara ameongeza, Rais wa TFF, Jamal Malinzi na vyombo vyake vya TFF wanataka kuharibu soka nchini.
JF.
No comments:
Post a Comment